Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia mamia ya wakazi wa Wilaya ya Magu,Mkoani Mwanza jana mchana.
Mamia
ya Wakazi wa Wilaya ya Magu wamkimsikiliza Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara mjini Magu jana Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akufunua kitambaa kushiria kweka jiwe la msingi katika jengo la Halmshauri ya mji wa Magu leo.Pembeni kulia ni Mkuu wa wilaya ya Magu Bi.Jacqueline Liana.Picha na Freddy Maro
Rais
Jakaya Kikwete ngoma ya utamaduni wilaya ya Magu kabla ya kuhutubia
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu
Rais
Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa wilaya ya Magu kwenye mkutano
wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha sabasaba mjini Magu. Picha na John Lukuwi
*****************************************
*****************************************
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa siyo kazi ya Serikali
kuviokoa vyama vya ushirika kutoka kwenye madeni kwa sababu shughuli za
ushirika ni za sekta binafsi na mali ya wanachama wenyewe.
Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa ni
jambo la kusikitisha kuwa makosa ya ushirika na wezi wa baadhi ya viongozi wa
vyama vya ushirika hatimaye yanabebeshwa vyama vya siasa.
Kama namna ya kuwasaidia wananchi,
Rais Kikwete amewataka viongozi mbali mbali wa mikoa kuwasaidia wananchi ili
kupata viongozi waadilifu na waaminifu na wala siyo wezi kama ilivyo sasa kwa
vyama vingi vya ushirika.
Rais Kikwete ameyasema hayo usiku
wa kuamkia leo, Jumamosi, Septemba 7, 2013, wakati alipopokea Ripoti ya
Maendeleo ya Mkoa wa Mwanza kwenye Ikulu Ndogo mjini Mwanza kwenye siku ya
kwanza ya ziara yake ya siku tano mkoani humo.
Rais Kikwete aliwaambia viongozi
hao wa Mkoa wa Mwanza: “Tumewahi huko nyuma kulipa madeni yote ya vyama vya
ushirika. Nia ilikuwa kuvisaidia vyama hivyo na wanachama wake kujipanga upya
na kupata uhalali wa kuweza kukopa fedha za kjuendesha shughuli zao. Lakini
sasa, vyama hivyo, vimerudi kule kule kwenye madeni.”
Alitoa mfano wa Chama cha Ushirika
cha Mkoa wa Pwani kama moja ya vyama vya ushirika ambavyo madeni yake yalilipwa
na Serikali lakini sasa kina deni kubwa zaidi kuliko hata lile lililolipwa na
Serikali.
“Wale watu wa Pwani walikwenda
kukopa na benki moja ikakubali kuwapa fedha. Wameshindwa kulipa na ule ushirika
nadhani utakufa. Njia bora kwa vyama vya namna hiyo ni kuviachia vife tu kwa
sababu havina faida yoyote kwa mkulima.”
Aliongeza: “Vyama vya ushirika siyo
mali ya Serikali. Ni mali ya wanaushirika na hivyo ushirika ni sekta binafsi.
Lakini hakuna shaka kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wanatesa
wananchi. Wanakopa fedha kwenye mabenki lakini wanashindwa kuzirudisha fedha
hizo na hilo linapotokea Serikali inalaumiwa kwa hali hiyo.”
Rais alikuwa anatoa maelekezo yake
baada ya kuambiwa kuwa Chama cha Ushirika cha Nyanza cha Mkoa wa Mwanza kilikuwa
kinakamilisha mpango wa kukopa kiasi cha sh bilioni saba kutoka Benki ya
Raslimali Tanzania (TIB) kwa ajili ya kununulia pamba.
Lakini aliwaambia viongozi hao:
“Uamuzi wa kukopa ama kutokukopa ni wa kwenu. Nyanza ni mali yenu, wezi
waliopata kukibebesha madeni chama hicho mliwachagua nyie wenyewe. Fedha ni
zenu lakini hatimaye athari za makosa yenu yanaiathiri Serikali na hata vyama
vya siasa.”
“Kuna wakati viongozi wa Chama cha Nyanza walipata
kuuza godown ya thamani y ash milioni 600 kwa sh milioni 50 tu. Hawa ni wezi wa
mchana wanaoiba kweupe. Wanaiba lakini wanataka Serikali iwasaidie. Kwa nini?
Nadhani kazi yetu kama viongozi ni kuwasaidia wananchi kupata viongozi adilifu
na aminifu siyo wezi,” alisema Mheshimiwa Rais Kikwete na
kuongeza:
“Tatizo ni kwamba hata sisi
viongozi tunakataa kuwashughulikia wezi kwa sababu hawa ni watu maarufu na
wakati mwingine baadhi ya viongozi wanakula nao na jambo hilo limekuwa tatizo
kubwa sana. Tunavifikisha vyama vya ushirika mahali ambako sina uhakika kama
bado ni mali ya wakulima. Wakulima wanakutana na ushirika wakati wa kuchagua
viongozi tu na baada ya hapo wakulima hawaonekani tena.”
Post a Comment