Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Mbeya
WEKUNDU
wa Msimbazi Simba SC, Chini ya kocha wake Abdallah Kibadeni “King
Mputa” , kwa mara nyingine tena wamewatambia Wazanzibar baada ya
kuwazamisha mabao 2-1 mabingwa wa Zanzibar KMKM katika mchezo wa
kirafiki uliofanyika jioni ya leo dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Bao
la kwanz la Simba lilifungwa katika dakika ya 28 na nyota wake Said
Ndemla baada ya kupokea pande maridadi kutoka kwa Issa Rashid “Baba
Ubaya”
Mnyama
alitinga tena nyavuni katika dakika ya 41 baada ya beki wake, Mrundi,
Gilbert Kaze kupiga shuti la moja kwa moja kufuatia kiungo mwenye uwezo
mkubwa wa kupiga chenga ama kupiga rangi mpira, Ramadhan Chombo “Redondo
wa Kibongo” kufanyiwa madhambi.
KMKM
chini yakocha wake, Ally Bushiri ilipata bao lake la kusawazisha katika
dakika ya 54 kupitia kwa Iddi Kambi aliyetumia maarifa makubwa kuizidi
ngome ya simba na kuandika kimiani bao hilo.
Licha
ya kufungwa na Simba, KMKM imecheza soka zuri na la kufundisha na
kuonesha wazi kuwa wamekomaa na wanastahili kutwaa ubingwa wa ligi ya
visiwani Zanzibar.
Septemba
2 mwaka huu, Simba ilicheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Mafunzo
ya Zanzibar na kushinda mabao 4-3, lakini mchezo huo pia ulikuwa
maalumu kuwatambulisha wachezaji wapya, Henry Joseph Shindika, Gilbert
Kaze na Amisi Tambwe ambao hawakutambulishwa siku ya “Simba Day”.
Lakini
Henry Joseph hakucheza kufuatia kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa
ya Tanzania, Taifa Stars kinachotarajia kushuka dimbani kesho mjini
Banjul nchini Gambia, mchezo wa kukamilisha ratiba wa kuwania kufuzu
fainali za kombe la Dunia huko Brazil mwakani.
Sasa
Mnyama anajiandaa na mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara, Septemba 14
dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kikosi
cha Simba SC leo: Andrew Ntalla, Haruna Shamte, Issa Rashid ‘Baba
Ubaya’, Hassan Hatibu, Kaze Gilbert, Abdulhalim Humud, Twaha Ibrahim,
Said Ndemla, Amisi Tambwe, Ramadhani Chombo ‘Redondo’/Betram Mombeki na
Zahor Pazi.
KMKM;
Mudathir Khamis, Kassim Nemshi, Faki Hamad, Iddi Mgeni, Khamis Ali,
Ibrahim Khamis, Nassor Ali, Abdi Kassim ‘Babbi’, Ally Ahmed ‘Shiboli’,
Mwinyi Ameir na Iddi Kambi.
Post a Comment