Wachezaji
wa Timu ya Taifa (Taifa Stars) wamerejea nyumbani baada ya mechi yao na
Gambia ambapo walifungwa 2-0 huku matarajio yote sasa yakiwa ni kufuzu
kucheza Kombe la Afrika 2015.
Wachezaji
hao 18 pamoja na benchi la ufundi waliwasili katika Uwanja wa Ndege wa
Julius Nyerere saa nane mchana kwa ndege la shirika la Kenya.
Hii ni
mechi ambayo Taifa Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager,
ilitakiwa kushinda lakini ilikosa wachezaji tisa muhimu ambapo baadhi
yao hawakuruhusiwa na vilabu vyao na wengine walikuwa majeruhi.
Akizungumza
baada ya kuwasili kocha Kim Poulsen alisema kuutkana na hali halisi
alilazimika kuwachezesha wachezaji vijana ambao uzoefu wao sio mkubwa
sana kama ule wa wachezaji wa kawaida ambao mara nyingi huwa wanaanza.
“Tumesikitishwa
na matokeo haya lakini kama nilivyosema Gambia waliita wachezaji wao
wote wanaocheza nje lakini sisi tulikosa timu karibu nzima….vijana
waliocheza walijitahidi lakini wenzetu waliwazidi uzoefu,” alisema.
Alisema
ni muhimu watanzania watambue kuwa mechi za kufuzu kucheza kombe la
dunia zimekuwa muhimu sana kwa Tanzania kwani wachezaji wengi
wametambulika na wameitwa nje. “Kuna wachezaji kama Shomari kapombe,
Mwinyi Kazimoto, ambao kutokana na mechi hizi wamepata nafasi ya kwenda
kucheza nje,” alisema.
Kocha
huyo alisema yuko makini sana kutekeleza mpango wa muda mrefu ambao ni
kuhakikisha Tanzania inafuzu kucheza Kombe la Afrika 2015,” alisema na
kuongeza kuwa timu anayoendelea kujenga itafanya kazi hiyo.
Alisisitiza
kuwa ni lazima TFF ihakikishe wachezaji wote muhimu wanakuwepo wakati
mechi za kufuzu kucheza Kombe la Afrika zitakapoanza mwakani.
“Kwa
sasa wachezaji watarudi vilabuni kwao na baada ya muda mfupinitawaita
tena ili tujiandae na Mashindano ya CECAFA Senior Challenge
yatakayofanyika Nairobi,” alisema.
Aliwataka watanzania wawe na subira kwani ana imani na timu anayoijenga.
Akiunga
mkono maneno ya Poulsen, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager,
George Kavishe, ambaye bia yake inadhamini Taifa Stars, alisema ni
lazima nguvu zote zielekezwe katika AFCON 2015.
“Tungefurahi
kama tungefuzu kucheza Kombe la Dunia lakini ni mapema sana kwa timu
yetu ambayo bado inajengwa…tumpe kocha nafasi aweze kutimiza haya
malengo na sio kumkatisha tama,” alisema.
Alisema
wao kama wadhamini wanafarajika na mabadiliko mbalimbali yaliyofanyika
katika Timu ya Taifa tangu waanze kuidhamini Timu hiyo mwezi Mei mwaka
uliopita.
Post a Comment