Rais
na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
akivishwa skafu kutoka kwa chipukizi mara tu baada ya kuingia wilayani
Sengerema kwa ziara ya siku moja tarehe 10.9.2013.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Katunguru
kilichoko wilayani Sengerema alipokwenda kijijini hapo kwa kwa ajili ya
kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa Katunguru/ Nyamtelela
tarehe 10.9.2013.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji wa
Katungulu/Nyamtelela utakaogharimu shs milioni 734 na utawanufaisha
zaidi ya watu elfu kumi.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Luchili akiwa
njiani kwenda katika kijiji cha Bukokwa kuzindua rasmi mradi wa umeme
tarehe 10.9.2013.
Wageni
waalikwa wakifuatilia kwa makini sherehe za uzinduzi wa mradi wa umeme
vijijini uliofanywa na Rais Kikwete huko Bukokwa wilayani Sengerema
tarehe 10.9.2013.
Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akipokea hati ya
makabidhiano ya mradi wa umeme wa Bukokwa uliofadhiliwa na Millenium
Challenge Co-operation ya Marekani.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete akizindua rasmi mradi wa umeme wa Bukokwa tarehe 10.9.2013
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi katika mradi wa maji
Katika kijiji cha Katunguru/Nyamtelela wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza
leo.Kulia ni Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe.
Mwakilishi
wa Serikali ya watu wa Marekani Bwana Karl Fickenscher akitoa hati ya
kukabidhi mradi wa MCC I kwa waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo wakati wa hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme
kwenye mifumo ya kusambaza umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika
katika kijiji cha Bukokwa wilayani Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Katikati
akishuhudia ni Afisa mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge
Account-(MCC)Tanzania Bwana Bernard Mchomvu.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utekelezaji wa mradi wa
umeme wa MCC unaotekelezwa katika mikoa ya Mwanza na Geita wakati wa
hafla ya ufunguzi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambaza umeme
mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha Bukokwa wilyani
Sengerema,Mkoani Mwanza leo.Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa
Sospeter Muhongo.
Mwakilishi
wa Millenium Challenge Account nchini Tanzania Bwana Karl Fickenscher
akipanda mti wa kumbukumbu muda mfupi baada ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete kuzindua mradi wa njia mpya za umeme kwenye mifumo ya kusambazia
umeme mikoa ya Mwanza na Geita uliofanyika katika kijiji cha
Bukokwa,Wilayani Sengerema leo. Kushoto ni Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete na kulia ni Waziri wa Nishati na madini Profesa Sospeter
Muhongo(picha na Freddy Maro)
PICHA NA JOHN LUKUWI
Post a Comment