UONGOZI
wa hospitali ya Mbagala Rangitatu (Zakhem) iliyopo jijini Dar es
Salaam umesema kwamba si kweli mama mjamzito alifukuzwa usiku wa
manane kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila siku la hapa
nchini hivi karibuni.
Kauli hiyo
ilitolewa leo na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo,Dk. Julius
Nyakazilibe katika taarifa yake kwa vyombo baada ya uchunguzi wa tukio
hilo kufanyika,ambao umehusisha mama mjamzito huyo wakiwemo ndugu wa
mlalamikaji ikiwemo nesi wa na daktari wa zamu.
Ambapo
alisema Mei 31, mwaka huu mama huyo mjamzito ,Ashura Omary alifika
hospitalini hapo majira ya saa sita usiku akiwa na ndugu
zake walimkuta nesi wa zamu kwenye wodi ya wakina mama, lakini kabla ya
kupokelewa aliingia mama mwingine mjamzito mwenye kifafa cha mimba.
“
Kutokana na sababu za kiutaalamu nesi wa zamu alianza kumuhudumia mama
mwenye kifafa cha mimba, hali hiyo ilimfanya Ashura kuanza
kulalamika kuwa hakuhudumiwa wakati yeye alikuwa wa kwanza kuingia.
Kitendo hicho kilimfanya nesi huyo amweelekeze wodini kupumzika na
kusubiri.
Dk.
Nyakazilibe alifafanua kuwa Ashura alipofika wodini alikuta vitanda
vyote vimejaa na kukosa mahali pa kulala ambapo aliendelea kusimama
akimsubiri nesi,baada ya muda nesi huyo alienda kumpima na kumwambia
njia yake haijafunguka na uchungu haujaanza,hivyo alimwambia aende
nyumbani na kurudi siku inayofuata yaani saa tano asubuhi .
Alisema
baada ya kuambiwa hivyo Ashura alitoka nje na kumwambia mama yake
aliyekuwa amemsindikiza kilichotokea ndani huku akimlaumu kuwa kwa nini
walimleta hopitalini hapo wakati tangu awali alitaka kwenda
kujifungua kwenye kituo cha Mbagala Kizuiani (Round table).
Baada
ya majadiliano kati ya mgonjwa na ndugu waliomleta walikubaliana
kuondoka na kwenda Mbagala Kizuiani usiku huohuo. Hivyo nesi wa zamu
alipomaliza kumuhudumia mama mwenye kifafa aliingia wodini ili
amuhudumie lakini alimkuta hayupo alipouliza wagonjwa wengine walisema
ametoka nje kuongea na ndugu zake .
Alisema nesi huyo aliamua kumtafuta nje lakini hakumkuta mama huyo wala ndugu zake.
Aidha
Dk. Nyakazilibe alisema kutokana na maelezo hayo mama huyo aliondoka
mwenyewe kitendo kilichotafsiriwa kuwa hakutendewa haki na kusema kuwa
amefukuzwa.
Kuhusu
tuhuma ya mtoto mchanga kunyeshwa dripu ya maji Agosti 15, mwaka huu,
alisema si za kweli kwani mtoto huyo hakuwa mchanga bali ana umri wa
miaka miwili.
“
Si kweli kuwa mtoto alinyeshwa maji ya dripu bali alipewa matibabu ya
ORS(Oral Rehydration Salt). Mama aliagizwa kununua maji safi ili yaje
kuchanganywa na dawa iliyotumika kumnyeshwa mtoto huyo baada ya kuona
mgonjwa na uwezo wa kunywa maji wakati wauguzi wakiendelea kutafuta
mishipa.
Aliongeza kuwa utaratibu huo ulifanyika kwa sababu za kiutaalam.
Uongozi
wa hospitali hiyo umewataka wananchi yanapotokea malalamiko yoyote
hospitalini hapo kutoa taarifa mara moja na si kusubiri muda upite. Pia
umewataka waandishi wa habari kupata maelezo ya kina wanapoandika
habari.
Post a Comment