TANZANIA ndiyo nchi inayoongoza kwa tafiti za kisayansi
ambazo zimewezesha kugunduliwa aina mpya 19 za kahawa, imebainika.
Meneja Mipango wa Taasisi ya Utafiti wa zao la
Kahawa Tanzania (TaCRI), Jeremiah Magesa alisema ugund
uzi huo umeifanya Tanzania kuwa ya juu zaidi katika teknolojia ya kahawa duniani.
uzi huo umeifanya Tanzania kuwa ya juu zaidi katika teknolojia ya kahawa duniani.
Magesa alisema juhudi hizo ndizo zimewezesha TaCRI
kupewa kombe na cheti mwaka 2011 kwa ugunduzi wa kahawa bora yenye
muonjo wa ladha nzuri zaidi katika ukanda wa Mashariki mwa Afrika.
Mkuu wa Kitengo cha Uboreshaji wa zao la Kahawa
TaCRI, Deusdedit Kilambo alisema kwa kawaida dunia ina aiana mbili za
kahawa ambazo ni Robusta na Arabika.
Kutokana na tafiti wa zao hili anasema waligundua
aina mpya 15 za Arabika nne za Robusta, ambazo alisema zina tija zaidi
kwa mkulima kwa kuongeza mazao na hata ubora kwenye soko.
“TaCRI imekuwa ikiendesha programu kabambe
kuendeleza aina bora ya kahawa kwa kutafiti ili kupata aina zenye tija
zaidi kwa mkulima.” alisema.
Alisema aina zote hizo zina ukinzani dhidi ya
magonjwa ambayo yamekuwa hakiathiri uzalishaji wa zao hilo kama vile
chulebuni, kutu ya majani na mnyauko fuzari.
Kilambo alisema wakulima wakizingatia kanuni bora
za uzalishaji zinazotolewa na TaCRI, kwa kutumia aina hizo 19, Tanzania
inaweza kuwa kwenye nafasi ya juu duniani.
Tanzania ni ya 20 kwa uuzaji wa zao la kahawa
katika soko la dunia na ni ya tano katika Afrika, kwa mujibu wa takwimu
za mwaka 2012, zilizotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya zao la Kahawa
(ICO).
Brazili inaongoza duniani ikifuatiwa na Vietnam wakati katika Afrika, Ethiopia ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Uganda, Ivory Coast, Papua New Guinea na Tanzania ni ya tano. MWANANCHI.
Brazili inaongoza duniani ikifuatiwa na Vietnam wakati katika Afrika, Ethiopia ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Uganda, Ivory Coast, Papua New Guinea na Tanzania ni ya tano. MWANANCHI.
Post a Comment