Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wakili Israel Magesa kuagwa rasmi Leo Jumamosi 7/9/2013 Mnazi Mmoja kuanzia Saa 6

 


indexWakili Magesa aliyekuwa wa kampuni ya Mawakili ya Magesa &Co. Advocates.
  Wakili Magesa ni baba  mzazi wa Phares Magesa(MNEC), Kalimba Magesa, Makongo Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na baba Mkwe wa Mrs. Haika Lawere(Mkurugenzi – Mbezi Garden Hotel), Dr. Julius Keyyu (Mkurugenzi wa Utafiti- TAWRI) na Ndg. Charanga ( Mkurugenzi – Tanzania Aviation Training College).
  Marehemu ameacha mjane Rhoda Magesa na wajukuu 8.
  Wakili Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya Kisutu, Katibu wa bodi na Mwanasheria Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International – Tanzania Chapter, Mwenyekiti wa Lions Club -Singida, pia ni mmoja wa wanasiasa waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.
Enzi za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Mbeya, Kilimanjaro, Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, Wakili Magesa ni miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.
  Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na shughuli rasmi ya kuaga itafanyika Jumamosi tarehe 7/9/2013 kuanzia Saa 6-10 jioni, Dares Salaam na mazishi yatafanyika siku ya jumatatu  9/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top