SERIKALI
imewataka wasimamizi watakaosimamia mtihani wa kumaliza Elimu ya
Msingi kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya
juu, huku ikiwaonya wale watakaokiuka agizo hilo kuwa watachukulia
hatua za kisheria.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Philipo Mulugo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dar es Salaam kuhusu mtihani huo, ambao unaotarajiwa kufanyika Septemba
11 na 12 mwaka huu.
“Napenda
kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu
kwani Serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria mtu yeyote
atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani” alisema Mulugo.
Naibu
Waziri huyo alisema kuwa wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa
nawakishriki katika kuwasadia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye
mitihani yao.
Katika
mtihani huo jumla ya watahiniwa 868,030 wamesajiliwa kufanya mtihani
huo, kati yao wavulana 412,105 sawa na asilimia 47.47 na wasichana
455,925 sawa na asilimia 52.52.
Naibu
Waziri huyo aliendelea kusema kuwa kuna jumla ya watahiniwa 844,810
ambao wanatarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili kati yao
wavulana 400,335na wasichana 444,475. Wanafunzi 22,535 kati yao wavulana
ni 11,430 na wasichana ni 11,105 watafanya mthani huo kwa lugha ya
Kiingereza ambao ndio waliyokuwa wakiitumia kujifunzia.
Kwa
upande wa watahiniwa wasioona, waliosajiliwa kufanya mtihani huo ni 88
wakiwemo wavulana 56 na wasichana 32. Watahiniwa wenye uoni hafifu ambao
huhitaji maandishi makubwa ni 597. Wanaotarajiwa kufanya mtihani kwa
lugha ya Kiswahili ni watahiniwa 546 kati yao wavulana ni 263 na
wasichana ni 283. Wanaotarajiwa kufanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza
ni watahiniwa 51 kati yao wavulana ni 21 na wasichana 30.
Aidha,
Mulugo alisema kuwa maandalizi yote kwa ajili nya mtihani huo
yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mtihani,
kusambazwa kwa fomu maalum (Optical Mark Reader, (OMR) za kujibia
mtihani na nyaraka zote muhimu zinazohusika.
Akijibu
swali lililoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano huo juu ya
watahiniwa kutumia fomu za OMR kujibia mtihani Naibu Katibu Mtendaji
Baraza la Mitihani Tanzania Dkt. Charles Msonde alisema kuwa wanafunzi
wameandaliwa vizuri kutumia fomu hizo na zimeonesha mafanikio makubwa.
Dkt.
Msonde alisema katika kipindi cha mwaka 2012 fomu zote zilizotumika
kujibia mtihani huo zilipita vizuri kwenye kompyuta na ambazo ziligoma
kutokana na sababu mbalimbali zilisafishwa na kunyooshwa na hatimaye
kukamilika na kusahihishwa.
Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi ,Hisabati na maarifa ya jamii.
Post a Comment