Mkuu
wa Ofisi ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dodoma, Nima Sitta
akihimiza utunzaji wa matenki ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwa
katika shule za msingi wilaya ya Singida na Ikungi. Shirika la WFP
limetoa shilingi 95,271,600 kugharamia ujenzi wa matenki hayo.(Picha na
Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Shirika
lisilo la kiserikali la Mpango wa chakula duniani (WFP) limetoa msaada
wa pampu 210 za maji zenye thamani ya zaidi ya shilingi 94 milioni kwa
shule za msingi na vikundi mbalimbali mkoani Singida.
Pampu hizo ni kwa ajili ya kilimo cha umwangiliaji bustani.
Hayo
yamesemwa juzi na Mkuu wa Ofisi ndogo ya WFP Dodoma Nima Sitta,wakati
akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matenki 12 ya kuvunia maji
ya mvua yaliyojengwa kwenye shule sita za wilaya ya Singida na wilaya ya
Ikungi.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Igaruri
wilaya ya Singida.
Alisema
lengo kuu la msaada huo wa pampu za maji,ni kila shule za msingi na
vikundi vya vijana,kuanzisha kilimo cha umwangiliaji maji bustani.
Nima
alisema kila shule ya msingi yenye chanzo cha maji,itapatiwa pampu si
chini ya mbili,wakati vikundi vya vijana waliomaliza elimu ya msingi na
wale waliomaliza kidato cha nne,watapatiwa si chini ya pampu tatu.
“Kwa
upande wa vijana,kila kikundi kinatakiwa kumiliki ekari sisizopungua
tatu na wawe wamejipanga vizuri,shule za msingi zimepewa sharti la kuwa
na shariti la kumiliki ekari mbili.Hivi sasa tunaendelea kuzizungukia
shule ili zile zenye sifa,ziweze kukabidhiwa pampu mapema
iwezekanavyo”alifafanua Nima.
Katika
hatua nyingine,Nima alitumia fursa hiyo kulipongeza shirika lisilo la
kiserikali la SEMA la mjini Singida, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa matenki
ya kuvunia maji na inayofanana na thamani ya fedha zilizotumika .
“Kwa
kweli SEMA kazi yao ni nzuri mno,wametekeleza kwa kiwango cha juu yale
yote ambayo yapo kwenye mkataba na kufanya mazuri zaidi baadhi ya
shughuli ambazo hazipo kwenye mkataba.Nisema tu kwamba kazi ya
SEMA,inapaswa kuigwa na wajenzi wengine kwa maendeleo ya
wananchi”,alisema.
Post a Comment