Makamu
wa Pili wa Rais was Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akibadilishana mawazo
wa Ujumbe wa Serikali ya Sharjah ambao upo Zanzibar kwa siku mbili
kuangalia maeneo ya uwekezaji vitega uchumi.
*****************************************
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inaendelea kukaribisha wawekezaji vitega
uchumi kutoka mashirika,Taasisi na Mataifa washirika katika mpango wake
wa kuimarisha uchumi wake pamoja na kuongeza pato la Taifa sambamba na
ustawi wa Wananchi wake.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati
akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Sharja ukiongozwa na Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Bandari Mhandisi Rashid Al Leem ambao upo Zanzibar kwa ziara
ya siku mbili kuangalia mazingira ya uwekezaji Vitega Uchumi hapa
Nchini.
Balozi
Seif alisema Zanzibar imeanza harakati za kuujengea uwezo uchumi wake
tokea mwanzoni mwa miaka ya 90 kwa kuimarisha miundo mbinu ili
kuuwezesha uchumi wa Visiwa hivi kuacha kutegemea zao moja la karafuu.
Alisema
hatua hiyo ya Serikali imelenga kutoa fursa zaidi kwa washirika na
Taasisi hizo kuunga mkono mpango huo kwa lengo la kuongeza nafasi za
ajira kwa kupunguza umaskini miongoni mwa wananchi.
“
Zanzibar ni eneo safi kimazingira katika masuala ya uwekezaji. Ni eneo
na amani, likizunguukwa na mandhari nzuri ambazo muwekezaji anaweza
kulitumia kwa uwekezaji wa miradi ya kiuchumi na maendeleo “.
Alisisitiza Balozi Seif.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza Ujumbe huo wa Serikali ya Sharjah
kwamba Zanzibar pia ina mtazamo wa kuwa na shirika lake ya Ndege
katika muelekeo wa kuongeza mapato zaidi.
Alisema
Makampuni ya Sharjah kupitia wataalamu wake wana fursa ya kufanya
utafiti wa kuingia ubia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika
uwekezaji wa sekta ya anga ambayo itasaidia kutoa huduma za usafiri
ndani ya ukanda wa Mashariki na kusini mwa Bara la Afrika.
Balozi
Seif alifahamisha kwamba Historia ya kibiashara inaonyesha kwamba
Zanzibar imekuwa kituo kikuu cha biashara katika karne kadhaa zilizopita
hali ambayo inaweza kurejea katika uhalisia wake endapo mipango hiyo
itakamilika hapo baadaye.
Aliupongeza
Ujumbe huo wa Serikali ya Sharjah kwa uwamuzi wake wa kuangalia
mazingira ya uwekezaji hapa Zanzibar suala ambalo linaonyesha
ushirikiano na uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili.

Mapema
Kiongozi wa Ujumbe huo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari ya Sharjah
Mhandisi Rashid Al Leem alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Balozi Seif kwamba Sharjah itaongeza ushirikiano wake na
Tanzania na Zanzibar kwa ujumla.
Mhandisi
Rashid alisema Serikali ya Sharjah iko tayari kutoa mafunzo mbali
mbali kwa vijana wa Zanzibar, kuwekeza katika miradi tofauti pamoja na
kuangalia uanzishwaji wa miradi ya pamoja kati ya mashirika na makampuni
ya pande hizo mbili.
Alifahamisha
kwamba Zanzibar imefanikiwa vyema katika uimarishaji wa miundo mbali
mbali inayotoa kichocheo kwa makampuni mbali mbali Duniani kushawishika
kutaka kuwekeza miradi yao Nchini.
“
Zanzibar imeendelea vyema na miundo mbinu iliyojiwekea hasa katika
sekta za ardhi na huduma za maji zinazotoa ushawishi kwa wawekezaji wa
ndani na nje ya Zanzibar kuwa na hamu ya kutaka kuwekeza Vitega uchumi
vyao “. Alifafanua Mhandisi Rashid Al Leem.
Mkurugenzi
huyo wa Mamlaka ya Bandari ya Sharjah alieleza kwamba Makampuni
yapatayo 12,000 ya Nchi hiyo tayari yameshatia saini mikataba ya
kuendeleza miradi katika mataifa tofauti Barani, Ulaya, Marekani, Asia
ambapo Sudan iliyomo Barani Afrika imebahatika kupata miradi ya mafunzo
tofauti.
Ujumbe
huo wa Viongozi Sita wa Serikali ya Sharjah umekuja Nchini kwa mualiko
wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh.
Mohammed Aboud Mohammed alipotembelea nchi hiyo hivi karibuni.




Post a Comment