Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani
Nchini (Necta),Dk Joyce Ndalichako, ameanza likizo ya mwaka mmoja kwa
kile kilichoelezwa kuwa anafanya utafiti juu ya uendeshaji wa mitihani
nchini.
Akizungumza na Mwananchi jana, Dk Charles Msonde ambaye ndiye anayekaimu nafasi ya Katibu Mtendaji wa Necta, alisema Dk Ndalichako amechukua likizo ya mwaka mmoja kwa ajili ya kufanya utafiti huo.
Dk Msonde alisema kuwa, likizo ya Dk Ndalichako ilianza Oktoba Mosi mwaka huu na itamalizika Septemba mwakani.
"Amechukua sabbatical leave, kwa wanataaluma ama watu walio kwenye ngazi kama zetu wanaweza kuchukua likizo kama hii. Yeye atakuwa anafanya utafiti unaohusu uendeshaji wa mitihani hapa nchini na pia ataangalia mambo ya matumizi ya alama za maendeleo za mwanafunzi (continuous assessment – CA)," alisema Dk Msonde.

"Utafiti huo utakuwa na manufaa kwa
shirika na kwa kuwa yeye ni Rais wa Mabaraza ya Mitihani Afrika atapata
nafasi ya kuangalia wenzetu wanafanya nini, kwa hiyo utafiti wake
ataufanya ndani na nje ya nchi. Utafiti huu utakuwa na manufaa kwa
baraza na nchi nzima."
Agosti mwaka huu Mwananchi ilifanya mahojiano Maalumu na Dk Ndalichano ambapo alizungumzia vitu mbalimbali ikiwamo kile alichosema ni tishio kwa Necta.
Alisema kuwa,kitu ambacho anaona ni tishio kwa baraza hilo ni mitizamo ya watu ambao kwa kiasi kikubwa wanakataa ukweli.
"Suala la ukweli unataka lisiwe kweli, mimi naona hiyo ni hatari mbaya zaidi, huwezi kutibu tatizo bila kujua ukweli, ili tuweze kuboresha elimu lazima tukubali ukweli na kujirekebisha," alisema Dk Ndalichako.
Alizungumzia pia ubora wa mitihani na kusema, mitihani inayotungwa na Necta ubora wake upo juu pamoja na usahihishaji wake.
Alisema mfumo wa kila mwalimu anasahihisha swali lake ni wa kipekee na Tanzania ni moja kati ya nchi za mwanzo kutumia mfumo huo.
"Kuna nchi mtu anapewa burugutu la mitihani ya watoto anaenda nayo nyumbani kusahihisha akishamaliza analeta majibu kisha watoto wanatangaziwa. Sisi mfumo wetu ni bora na sijui kwa nini watu wanakuwa na mtizamo hasi na Necta, sifa kubwa ya baraza lolote lile la mitihani ni kutoa majibu yanayofanana na hali halisi ya elimu ilivyo" alisema.
"Kwetu sisi tunachotaka siku zote kuona mtu anapewa kile anachostahili, watu wengine wanasema mitihani inayotungwa na kupewa watoto wote siyo sawa kwa sababu kuna baadhi ya shule walikuwa hawana walimu au vitabu, sasa swali la kujiuliza nani alitakiwa kutoa hivyo vitabu?" alisema Dk Ndalichako.
Chanzo>Mwananchi

Post a Comment