Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu enzi za uhai wake
Mwili
wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu utafikishwa nyumbani kwake eneo
la Sinza Mori lililoko jijini Dar es Salaam siku ya kesho Jumanne
October 29, 2013 kuanzia saa sita za mchana na mwili huo utaanza kuagwa
kwenye mida ya saa nane za mchana na baada ya kuagwa mwili huo
utafanyiwa maandalizi ya kusafirishwa kwenda
Zanzibar siku ya Jumatano asubuhi tarehe 30, October 2013 na mwili wa
marehemu ukifika Zanzibar, Unguja utapelekwa kanisani kwa ajili ya
maombi pia utapumzishwa kwenye makazi yake ya daima eneo la Mbozini,
Unguja siku ya Jumatano October 30, 2013
Balozi David Kapya akisaini kitabu cha maombolezo ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu nyumbani kwake eneo la Sinza Mori jijini Dar es salaam leo Jumatatu October 28, 2013
Mke wa marehemu akiwa kwenye majonzi
Wema Sepetu akiwasiliana na ndugu na jamaa kwenye msiba wa baba yake marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu leo October 28, 2013
Mtoto wa maheremu na pia msemaji wa familia Aman Isaac Sepetu akizungumza na vyombo vya habari leo nyumbani kwa marehemu
Post a Comment