Daladala
aina ya Coster yenye namba za usajiri T.960 AQY inayofanya safari zake
za Kibwabwa mjini Iringa mara baada ya kugongana na gari aina ya Isuzu
Tipa, lenye namba SM 3363 katika Mlima wa Ipogolo eneo la Kisima cha
Bibi.
Taxi
ambayo nayo ilisababishiwa ajari ikiwa katika eneo la tukio, huku askari
polisi wakilinda usalama wa mali za abiria na baadhi ya vitu katika
eneo la tukio.
Wananchi wa mji wa Iringa wakitazama ajari hiyo katika mlima wa Ipogolo (Kisima cha Bibi).
Basi aina
ya Coster linalofanya ruti zake Kibwabwa Manispaa ya Iringa likiwa eneo
la tukio, baada ya kugongana na Roli Tipper na kusababisha ajali
iliyojeruhi zaidi ya watu 30.
ZAIDI ya
abiria 38 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari manne mjini
Iringa, baada ya Bus dogo la abiria aina ya Coster kufeli breki na
kuyagonga magari matatu, ajali ambayo imetokea majira ya saa saba mchana
wa siku ya jana.
Tukio hilo limetokea katika mlima wa
Ipogolo, eneo maarufu mjini Iringa kama "Kisima cha bibi", ambapo ajali
hiyo imesababisha majeruhi 38 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa
mkoani Iringa, huku chanzo cha ajali hiyo kikisemekana kuwa na kuferi
breki kwa Bus hilo la abiria,lenye namba T. 960 AQY na kuyavaa magari
matatu, gari kubwa aina ya Tipper Isuzu SM784 BNA la manispaa ya Iringa,
Tax pamoja na Hiace.Akizungumzia hali ya majeruhi wa tukio hilo , Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa Dr. Deogratius Manyama amesema wamepokea majeruhi 38, na waliolazwa ni 8 huku majeruhi watatu wakiwa na hali mbaya, na kuwa majeruhi wengi wameumia zaidi kichwani na kifuani, huku majeruhi 27 wakiruhusiwa kurudi nyumba kwao kutokana na kutokuwa na majeraha makubwa.
MWISHO
Chanzo:Oliver Motto
Post a Comment