MAHAKAMA ya Rufaa Oktoba 30 mwaka huu inatarajiwa kufanya kusikiliza
marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo katika kesi iliyokuwa
ikimkabili mwanamuziki Nguza Viki maarufu kama Babu seya na wanawe.
Baada ya hukumu hiyo, Babu Seya na mwanawe pamoja na wakili wao Mabere
Marando waliomba marejeo ya hukumu hiyo.
Marejeo hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jopo la Majaji watatu wa
mahakama hiyo ambao ni Nathalia Kimaro, Mbarouk Mbarouk na Salum
Massati. Katika hukumu hiyo iliyotolewa Februari 2010,mahakama hiyo
iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na mwanawe, Papii
Nguza huku ikimuwaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu,
na Francis Nguza.
Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu,
Dar es Salaam,iliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii
Kocha’, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka
na kulawiti.
Januari 27 mwaka 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,
Thomas Mihayo alitupilia mbali
rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu
iliyotolewa na aliyekuwa Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu,Addy Lyamuya ambaye aliwatia hatiani kwa makosa yote waliyokuwa
wameshitakiwa nayo Juni 25 mwaka 2004.
Babu Seya na wanawe walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto
wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti
watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika
maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam.
Post a Comment