KIBAKA mmoja aliyejulikana kwa jina la Chura jana alioja joto ya jiwe
kwa kushushiwa kipigo na madereva wa Bajaj baada ya kuiba tairi ya
Bajaj maeneo ya Bamaga jijini Dar es Salaam.
Baada ya kupewa kipigo kikali alikimbilia kwenye Bajaj na kukaa
ndani yake ambapo alivutwa lakini haikuwezekana kutolewa kutokana na
jinsi alivyokuwa amejishikilia kwa nguvu ndipo watu walipoamua
kumpeleka katika kituo cha polisi Mabatini. Tairi hilo lililoibiwa
halikupatikana.Habari/picha:Na Gladness Mallya
Post a Comment