Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa
akiwasili katika viwanja vya Shule ya Mtakatifu Antony's Mbagala tayari
kuendesha harambee ya kuchangia madawati kwa shule za Tarafa ya Mbagala
ambapo jumla ya Tsh. Milioni 222 zilipatikana. Picha na Emmanuel Shilatu
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akifungua zoezi la uchangiaji
wa harambee ya kupatikana kwa madawati ya Tarafa ya Mbagala ambapo
aliisihi sana jamii kujitoa ili kukamilisha mahitaji muhimu ambayo ni
changamoto kwa shule za kata pasipo kuisubiria mpaka serikali kufanya.
Mbunge
wa Kigamboni, Mhe. Faustine Ndugulile akiisihi sana jamii haswa Wazazi
kujenga mazoea ya kufuatilia kwa ukaribu elimu za Watoto wao mara kwa
mara.
Mbunge
wa Temeke, Mhe. Abbass Mtemvu akitoa ahadi yake ili kufanikisha
upatikanaji wa madawati mashuleni huku akisikilizwa kwa umakini mkubwa
na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa.
Mbunge wa Ilala, Mhe. Mussa Hassan Zungu alichangia milioni 5 katika harambee hiyo. Picha na Emmanuel Shilatu.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akipokea michango mbalimbali
ya wazazi wenye uchungu dhidi ya watoto wao wanaoketi chini mashuleni.
Picha na Emmanuel Shilatu
Wanafunzi nao hawakuwa nyuma kuchangia upatikanaji wa madawati ambapo jumla ya pesa Tsh. Milioni 222 zilipatikana.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwa vyeti mbalimbali kwa wahitimu kidato cha nne wa shule 12 wa sekondari za Tarafa ya Mbagala.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa alikabidhiwa zawadi na kamati ya maandalizi ambapo zawadi hiyo ilikabidhiwa na Mwenyekiti wa kamati
Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa akiwa kwenye picha ya pamoja na Waalimu wakuu wa shule za sekondari za Tarafa ya Mbagala, viongozi waliokuwepo pamoja na Wajumbe wa kamati ya maandalizi. Picha na Emmanuel Shilatu


Post a Comment