Waziri
wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano Prof. Mbarawa akifungua maonyesho
ya Tanzania Homes Expo. Kushoto ni Imani Kajula Mkurugenzi Mtendaji wa
EAG Group, Kulia ni Oscar Mgaya Afisa Mtendaji Mkuu wa TMRC. Wengine ni
viongozi wa Camel Cement and CAM Gas.
Sehemu ya umati wa watu wakitembelea watoa huduma za sekta ya nyumba.
NHC ambao ni kati ya wadau wakubwa wa sekta ya nyumba nao wapo.
Umati wa watu waliofika kutembelea maonyesho ya Tanzania Homes Expo.
Maonyesho
makubwa ya sekta ya nyumba yajulikanayo kama Tanzania Homes Expo
yamefunguliwa rasmi leo na Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Mawasiliano
Prof. Mbarawa. Akiongea baada ya kutembelea mabanda mbali mbali alisema ‘’
Inafurahisha kuona watoa huduma mbalimbali binafsi na wa serikali wako
hapa kutoa taarifa na kuonyesha masuluhisho mbali mbali ya ujenzi.
Napenda kuchagiza umuhimu wa kutumia Tehama katika kuboresha maisha ya
wakazi’’.
Mkurugenzi
Mtendaji wa EAG Group ambao ni waandaaji na wamiliki wa Tanzania Homes
Expo alisema ‘’ Ukuaji wa idadi ya watu na upatikanaji wa makazi havina
uwiano sawa, hii ni changamoto ambayo inaweza kutatuliwa kwa kuwawezesha
wananchi kuwa na makazi hivyo maonyesho ya Tanzania Homes Expo
yanawawezesha wananchi kukutana na kufahamu huduma au kupata ushauri wa
sekta pana ya makazi’’.
Maonyesho
ya Tanzania Homes yamedhaminiwa na CAM Gas, Camel Cement, African Life,
CRDB na NHIF.Maonyesho hayo yameanza tarehe 14 na yataisha tarehe 15.
Post a Comment