Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MATUKIO ZAIDI YA JINSI MAREHEMU JULIUS NYAISANGAH ALIVYOAGWA LEO KWENYE VIWANJA VYA LEADERS CLUB JIJINI DAR


 Msafara wa Magari ambao moja wapo (la mbele) likiwa limebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Julius Nyaisanga ukiingia kwenye viwanja vya leaders muda huu kwaajili ya wakazi wa jiji la Dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga kabla ya Kusafirisha Kwao Tarime Mkoani Mara



Baadhi ya Ndugu, Jamaa na marafiki wakibeba jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga Kwaajili ya kupeleka sehemu husika tayari kwa kutoa heshima za mwisho kwa wakazi wa jiji la Dar waliofika katika viwanja vya leaders muda huu


Sehemu Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Julius Nyaisanga litakapowekwa kwaajili ya wakazi wa jiji la dar kuweza kutoa heshima zao za mwisho kabla ya kusafirishwa kwenda Tarime Mkoani Mara


 Baadhi ya wakazi wa jiji la dar waliojitokeza katika viwanja vya leaders .


 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah aliewahi kuwa ni mmoja wa viongozi waanzilishi wa Kituo cha Radio One, akitokea Radio Tanzania (RTD).Marehemu Nyaisangah atakumbukwa sana kwa uwezo wake mkubwa wa kusoma Habari pamoja na vipindi vya muziki,Matamshi yake laini na ufasaha mkubwa wa lugha ya Kiswahili, vilimtofautisha kabisa na watangazaji wengine.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwasa ambaye alifanya kazi pamoja na Marehemu Julius Nyaisangah akitoa heshima za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  na Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Mh. Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.
Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam leo kushiriki Kuaga Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah.Wanaompokea ni Wajumbe wa Kamati ya Mazishi (kushoto) ni Aboubakar Liongo na kulia ni Teddy Mapunda.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. Mohamed Gharib Bilal akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP,Dkt. Reginard Mengi wakati akiwasili kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam kuungana na Waombolezaji wengine kuaga Mwili wa Marehemu Julius Nyaisangah
Picha zote na Josephat Lukaza wa Lukaza blog
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top