Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MISS TANZANIA APONGEZWA, AFANYIWA BONGE LA PARTY

Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Redds Miss Tanzania 2012 Brigitte Alfred (kulia) na Miss Tanzania wa sasa Happiness Watimanywa wakati wa sherehe ya Kumpongeza (Brigitte) kwa kushinda nafasi ya tatu ya taji la dunia la kipengele cha urembo wenye malengo maalum. Mrembo huyo aliwashinda warembo 127.Sherehe hiyo ilifanyika kwenye hotel ya Giraffe Ocean mwishoni mwa wiki.
 *******
Mwandishi wetu
Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred Lyimo amesema kuwa ushindi wake wa nafasi ya tatu katika kipengele cha urembo wenye malengo maalum katika mashindano ya Miss World mwaka huu ni wa  Watanzania wote.
Brigitte alisema hayo katika hafla ya kuagwa iliyoandaliwa na waandaaji wa mashindano ya urembo nchini, kampuni ya Lino International Agency iliyofanyika kwenye hotel ya Giraffe. 
 
Alisema kuwa amefarijika sana kushinda nafasi hiyo kwani ilishirikisha warembo wote walioshindana mwaka huu katika mashindano hayo. Alisema kuwa hakuwa kazi rahis kushika nafasi hiyo kwani kipengele hicho ushirikisha warembo wote.
 
“Namshukuru mama yangu,  Verdiana Mashingia ambaye alikuwa bega kwa began a mimi katika kuhakikisha mradi wangu wa ujenzi wa bweni la albino wa shule ya smingi Buhangija shinyanga unafanikiwa, pongezi pia kwa kamati ya Miss Tanzania na wadhamini, Redds,” alisema Brigitte.
 
"Ndoto zangu za kuitumikia jamii hazitaishia hapa, nitaitumikia na nitaendelea kuwasaidia Albino ambao wamenichagua kuwa barozi wao," alisema mrembo huyo.
 
Aidha Brigitte alimpongeza Hapiness na kumtaka atumie kipaji alichonacho na urembo wake wa asili kuitoa kimasomaso Tanzania kwenye mashindano ya mwakani.
 
Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim “Uncle” Lundenga alisema kuwa Brigitte amefanya kitu cha kihistoria Tanzania na kuzishinda nchi kubwa mbali mbali kama Uingereza, Ufaransa na nyingine nyingi.
 
Lundenga alisema kuwa wamefarijika kwa mafanikio hayo na ndiyo maana wameamua kufanya hafla hiyo ambayo ni ya kihistoria huku akiwapongeza wadhamini, Redds kwa kudhamini hafla hiyo. 
 
Alisema kuwa ni vigumu kuamini, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa fai yao inazidi kukuwa, tena kwa mafanikio tofauti na watu wanavyodhani.
 
“Mfano mzuri ni mama yake Brigitte alivyokuwa bega kwa bega wakati wote mwanaye alivyokuwa na taji, huu ni mfano wa kuigwa na tunaomba wazazi wafuate nyayo za mama huyu,” alisema Lundenga.
 
Lundenga alisema kuwa Brigitte ameleta changamoto kubwa kwa mrembo wa sasa Happiness Watimanywa katika mashindano yanayofuata ya urembo ya dunia.
 
"Brigitte amefanya vizuri japo hakufanikiwa kutwaa taji la dunia, kuwa namba tatu kwenye taji la mrembo mwenye malengo ambalo kuacha taji la dunia ili linafuatia, Brigitte anahitaji kupongezwa," alisema.
 
Alisema kuwa Brigitte ameonyesha ushujaa na kuwapita warembo kutoka mataifa makubwa dunia ambao walichuana kwenye mashindano hayo na yeye kufanikiwa kuingia hatua ya tatu bora kwenye taji hilo.
credit: Wazalendo 25
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top