
Nilipopokea mwaliko
kutoka Mfuko wa Pensheni (PSPF) ukiniomba kuhudhuria kwenye hafla fupi
ya chakula cha mchana pamoja na wadau wa tasnia ya sanaa na michezo
nchini, sikuelewa mara moja lengo la hafla hiyo lakini baada ya kufika
ukumbini na kupata ufafanuzi wa mabadiliko makubwa yaliyofanywa na PSPF
nikapata somo.
Kumbe PSPF sasa si
kwa watumishi wa umma pekee bali hata wanamuziki, waigizaji, wachezaji
na hata watu wengine waliokwenye sekta zisizo rasmi wanaweza kujiunga na
kufaidika na mafao yanayotolewa na mfuko huo.
Wadau wengi wa tasnia
ya sanaa na michezo walijitokeza kwenye halfa hiyo tukianza na
Elizabeth Michael Lulu, Mwanamitindo mwenye mafanikio makubwa ndani na
nje ya nchi, Flaviana Matata, Mtitu, Steve Nyerere, Nahodha wa timu ya
taifa ya soka wanawake Sophia Mwasikili na wadau wengine wengii...

Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata


Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina Martin
Meneja wa Mawasiliano, Masoko na Uenezi wa PSPF, Costantina
Martin anasema lengo kukukutana na wadau hawa ni kutambulisha kwao mpango wa
uchangiaji wa hiari (PSPF SUPPLIMENTARY SCHEME-PSS) ambao unamwezesha mtu
yeyote kujiunga na mpango huo awe ameajiriwa au amejiajiri mwenyewe.
“Uzuri wa mpango huu wa uchangiaji wa hiari, unaruhusu hata
wanachama waliokwenye mifuko mingine kujiunga nao lakini pia mwanachama
anayohiari ya kuhamia kwenye mpango wa uchangiaji kwa mujibu wa sheria yaani
Main Scheme” Anasema Costantina
Anasema kuwa kiasi cha michango kwenye mpango wa hiari
kinaanzia shilingi elfu kumi (10,000) kwa mwezi na hakuna kiwango cha juu
ambapo mwanachama yuko huru kuchagua kuwasilisha michango kwa wiki, mwezi au
kwa msimu na michango hiyo inawasilishwa kupitia akaunti ya benki, au wakala wa
malipo wa M-Pesa na Airtel Money.

Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu anasema mpango wa
hiari ni mkombozi kwa wadau wa sanaa na michezo kwa kuwa utawawezesha kujiwekea
akiba itakayowasaidia wakati na hata baada ya kustaafu kufanya shughuli zao.
Katika kuhakikisha kuwa elimu ya uhifadhi inawafikia watu
wengi na kuwahamasisha kujiunga na mpango huo waa hiari PSPF imekusudia
kuwafanya wasanii na wanamichezo kuwa mabalozi katika kufikisha elimu hiyo kwa
jamii.
“Sio jambo rahisi kuielimisha jamii juu ya kujiwekea akiba
kwa ajili ya maisha yao ya baadaye lakini kupitia wasanii na wanamichezo
tunaweza kuleta mabadiliko na kufanya watu wengi kuwekeza katika mifuko ya
hifadhi ya jamii” anasema Mayingu
Shuhudia picha za tukio zima la hafla ya chakula cha mchana kwa wadau wa sanaa na michezo iliyoandaliwa na PSPF.

Wadau wa sanaa

Afisa Mahusioano wa PSPF, Fatma Elhagy akiwa na mtumishi mwenzake

Afisa Mawasiliano na Masoko wa PSPF, Hawa Kikeke

Naibu Mkurugenzi wa Michezo, Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Juliana Yasoda


Mdau wa sanaa na akiwa na staa wa kesho

Wadau wa sanaa na michezo

Baadhi ya watumishi wa PSPF

Mshereheshaji katika hafla hiyo, Angela Bondo

Baadhi ya mameneja na wakurugenzi wa idara mbalimbali wa PSPF

Wadau

Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa miguu
kwa wanawake, Amina Karuma akiwa na Nahodha wa timu ya Taifa ya soka
kwa wanawake Sophia Mwasikili

Elizabeth Michael (Lulu) na Flaviana Matata


Mr. Tairo kutoka Bodi ya Filamu Tanzania

Mdau

Kocha msaidizi wa klabu ya Simba Jamuhuri Kiwelu Julio nae alikuwepo

Columba Samjela kutoka Umoja wa Washereheshaji

Meneja Matekelezo wa PSPF, Amin Labani

Kaimu Mkurugenzi Uendeshaji PSPF, Frances Mselemu

Muda wa maakuli

Mwendo ni 'kujisevia'


Wadau wa sanaa na michezo

Baadhi ya watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja
Post a Comment