Balozi
wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa kwanza kushoto) akiwa na Waziri wa
Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma ya Balozi) pamoja na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda
Bw. Guy Kalisa (mwenye tai nyekundu) wakikagua eneo la kituo cha pamoja
cha ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
Balozi
wa Japan Mheshimiwa Masaki Okada (wa pili) akiwa na Waziri wa Ujenzi
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (nyuma) pamoja na Afisa Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa
(wa pili kutoka nyuma) wakikagua eneo la kituo cha pamoja cha
ukusanyaji ushuru kwa upande wa Rwanda.
Injinia
Hitoshi Kameda (kushoto) akitoa maelezo kwa Balozi wa Japan Mheshimiwa
Masaki Okada (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli (wa pili kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Maendeleo ya Usafirishaji nchini Rwanda Bw. Guy Kalisa (kulia)
wakikagua eneo la ujenzi wa daraka la Rusumo kwa upande wa Rwanda.
Maporomoko
ya Rusumo katika Mto Kagera linapojengwa draja la kuziunganisha nchi za
Tanzania na Rwanda katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera.
|
Magari
yakipita katika daraja la zamani (kulia) ambalo linatumika hadi sasa na
kushoto ni ujenzi wa daraja jipya ukiendelea katika Mto Kagera eneo la
Rusumo
*****
Balozi
wa Japan nchini Tanzania Mheshimiwa Masaki Okada ameelezea kuridhishwa
na utekelezaji wa mradi ujenzi wa daraja la kimataifa la Rusumo na kituo
cha pamoja cha ukusanyaji ushuru katika eneo la Rusumo mpakani wa
Tanzania na Rwanda.
Miradi
hiyo miwili mikubwa inayofadhiliwa na Serikali ya Japan ilianza
kujengwa mwezi Machi mwaka huu wa 2013 na imepangwa kukamilika mwezi
Novemba mwaka 2014.
“Nimeridhishwa
na viwango na kasi ya utekelezaji wa mradi huu” alisema Balozi Okada
wakati alipotembelea eneo hilo la mpakani mwa Tanzania na Rwanda ambapo
alisisitiza kuwa, inatia moyo kuona fedha zilizotolewa na nchi yake
zikitumika vizuri kwa lengo la kukamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Naye
Meneja wa Tanroads wa Mkoa wa Kagera Injinia John Kalupale akitoa
taarifa kwa Balozi huyo wa Japan ambaye alifuatana na Waziri wa Ujenzi
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, alielezea kuwa uamuzi wa kujenga
daraja jingine katika eneo hilo la mpakani, unatokana na mahitaji halisi
ya wakati huu kwani daraja linalotumika hivi sasa lilijengwa miaka 40
iliyopita likiwa na uwezo wa kubeba tani 32.
Aliendelea
kueleza kuwa ingawa miaka ishirini baada ya ujenzi wa daraja hilo
kulifanyika ukarabati mkubwa kwa lengo la kuimarisha uwezo wake, bado
kumeendelea kuwepo kwa ongezeko kubwa la magari hasa yanayosafirisha
bidhaa kati ya Bandari ya Dar es Salaam na nchini jirani ya Rwanda.
Injinia Hitoshi Kamega ambaye ni Mhandisi Mkazi wa Kampuni mbili
zilizoungana kuusimamia mradi huo ambazo ni Chodei Co. Ltd. na Nippon
Koei Co, amelezea kuwa ujenzi wa daraja hilo la Rusumo lenye urefu meta
80 pamoja na kituo cha ushuru, unatekelezwa na Mkandarasi Daiho Co.
kutoka Japan kwa gharama ya Shilingi bilioni 31.736.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli hata hivyo alibainisha
kujitokeza kwa mapungufu katika baadhi ya maeneo ya mradi huo ambayo
wizara yake kwa kushirikiana na Ubalozi wa Japan hapa nchini
wanayafanyiakazi ili kuhakikisha kuwa kunakuwepo na uwiano mzuri wakati
wa utekelezaji wa mradi huo na pale huduma zenyewe zitakapoanza
kutolewa..
Waziri Magufuli aliyataja baadhi ya mapungufu hayo kuwa ni pamoja na
kutotengwa kwa eneo la kutosha la maegesho ya magari kwa upande wa
Tanzania na kuhitajika kwa upanuzi wa majengo ya huduma za kiutawala
hasa wakati wa kutekeleza mipango ya baadaye kwa kuzingatia ongezeko la
shughuli za kibiashara linavyoonekana katika eneo hilo.
PICHA NA MICHUZI BLOG
|
on Friday, October 25, 2013
Post a Comment