Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI

DSC00260
DIWANI ATHUMANI – ACP, KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
“PRESS RELEASE” TAREHE 15. 10. 2013.
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – MAUAJI.
MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO KATIKA MSITU WA IHONDO KIJIJI CHA MALANGALI KATA YA SWAYA MPAKANI MWA WILAYA YA MBEYA VIJIJINI NA WILAYA YA   RUNGWE MKOA WA MBEYA. MICHAEL S/O WILLIAD, MIAKA 24, MSAFWA, M/BIASHARA, MKAZI WA MALANGALI WILAYA YA  RUNGWE, ALIKUTWA AMEUAWA KWA KUKATWA MAPANGA KICHWANI NA MWILI WAKE KUTUPWA KATIKA MSITU WA IHONDO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA. MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVIZIA MAREHEMU AKIWA ANATOKA MBEYA MJINI KUNUNUA MAHITAJI/BIDHAA NDOGO NDOGO ZA DUKANI KWAKE AKIWA NA PIKIPIKI YAKE  T.819 CDQ AINA YA  T-BETTER NA KUMUUA KISHA KUMTUPA MSITUNI. PIKIPIKI YA MAREHEMU ILIKUTWA NJIANI IMEEGESHWA IKIWA NA BIDHAA ALIZOKUWA AMENUNUA. CHANZO KINACHUNGUZWA. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA JUU YA  MTU/WATU WALIOHUSIKA KATIKA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI WAKAMATWE NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.

WILAYA YA MBARALI – AJALI YA GARI KUMGONGA MPANDA BAISKELI NA
KUSABABISHA KIFO NA MAJERUHI
.
MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 07:15HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA META – IGURUSI BARABARA YA MBEYA/IRINGA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA. GARI T.404 AAT AINA YA TOYOTA MARK II LIKIENDESHWA NA DEREVA SAAD S/O MWATOVENE, MIAKA 71, MSANGA, MKAZI WA CHIMALA LILIMGONGA MPANDA BAISKELI REHEMA D/O KUNDAMA, MIAKA 21, MHEHE, MKULIMA, MKAZI WA MAPUNGA – IGURUSI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA MAJERUHI KWA ABIRIA WAKE DANIEL S/O GEORGE, MIAKA 21, MUWANJI, MKULIMA, MKAZI WA IGURUSI AMBAYE AMELAZWA HOSPITALI YA CHIMALA- MISHENI NA MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALINI HAPO. CHANZO NI MWENDO KASI. MTUHUMIWA AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA BHANGI.
MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA MAKONGOLOSI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO WALIMKAMATA RAMADHAN S/O JUMA, MIAKA 31, MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MAKONGOLOSI AKIWA NA BHANGI DEBE MOJA SAWA NA UZITO WA KILO 10. MTUHUMIWA NI MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA  MTUMIAJI.
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SILAHA [RIFFLE].
MNAMO TAREHE 13.10.2013 MAJIRA YA SAA 14:00HRS HUKO KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA LUKWATI WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI  WAKIWA DORIA/MSAKO  KWA KUSHIRIKIANA NA MAAFISA WA HIFADHI HIYO WALIMKAMATA SAMOLA S/O DAMAS, MIAKA 41, MBUNGU, MKULIMA, MKAZI WA KIJIJI CHA GUA AKIWA NA SILAHA BUNDUKI AINA YA  RIFFLE NA RISASI MBILI [02]. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHA TABIA YA  KUJIMILIKISHA SILAHA KINYUME CHA SHERIA NA BADALA YAKE WAFUATE TARATIBU ZILIZOWEKWA. 
WILAYA YA MBEYA VIJIJINI – KUFA MAJI.
MNAMO TAREHE 14.10.2013 MAJIRA YA SAA 13:30HRS HUKO MTO MBALIZI WILAYA YA MBEYA VIJIJINI MKOA WA MBEYA. MTOTO AITWAYE YUSUPH S/O TIMOTH, MIAKA 12, KYUSA, MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO [05] SHULE YA MSINGI IWINDI ALIFARIKI DUNIA KATIKA MTO HUO WAKATI ANAOGELEA. UCHUNGUZI WA AWALI UMEBAINI KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKISUMBULIWA NA TATIZO LA KIFAFA HALI ILIYOSABABISHA KIFO CHAKE WAKATI AKIOGELEA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI TEULE YA WILAYA – IFISI.  KAMANDA WA POLISI  MKOA WA MBEYA  KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI  ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWA MAKINI NA WATOTO WAO ILI KUWEZA KUEPUKA MADHARA/MATATIZO YANAWEZA KUWAPATA WATOTO WAO. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI WAISHIO MAENEO YENYE VYANZO VYA MAJI KUCHUKUA TAHADHALI KWA WATOTO WAO ILI KUEPUKA MADHARA YANAYOWEZA KUEPUKIKA.
   Signed by:
 [DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top