Bodi
ya utalii Tanzania(TTB)imezindua mpango mkakati wake wa miaka mitano wa
kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini huku ikieleza mkakati wa
kutafuta soko jipya la watalii nchi za China,Japani na Brazil.
Meneja
utafiti na maendeleo wa TTB Deogratus Malingo akieleza mkakati huo wa
TTB katika mkutano na kampuni zinazotoa huduma ka watalii mkoani Arusha
alisema TTB imejipanga kuboresha mfumo wa kutangaza Tanzania kam,a moja
ya vituo bora vya utalii duniani.
Malongo
alisema ingawa idadi ya watalii wanaokuja nchini imekuwa ikiongezeka
kwa kila mwaka na kufikia 1.2 bado kuna haja ya kuendelea kutangaza
vivutio bora vya utalii katika nchi ambazo zinaleta watalii na nyingine
ambazo bado watalii wanaofika ni wachache.
“Kwa
sasa waingereza ndiyo wanaongoza kwa kutembelea Tanzania mwaka jana
walikuwa 69,680wakifuatiwa na wamarekani65,110na Waitaliano 50,187
lakini kuna haja ya kujitangaza zaidi nchi hizi na nyingine
duniani”alisema Malongo.
Akizungumza
katika mkutano huo mwenyekiti wa chama cha watoa huduma za utalii
Tanzania(TATO)Willy Chambulo alisema sekta hiyo bado inakabiliwa na
changamoto nyingi.
Chambulo
alisema kuna urasimu wa kupata vibali gharama kubwa za watalii
wanaokuja nchini na kukosekana ndege ya moja kwa moja kutoka mataifa
makubwa kama china na kwengineko duniani na kuna haja kwa serekali
kuliangalia hilo.
“tunaamini
serekali ikifanyiakazi tutaweza kuongeza idadi ya watalii na kuongeza
pato la taifa na kuna haja ya kuweka mazingira mazuri ya kuweza kupata
usafiri wa uhakika kutoka mataifa hayo ilikuweza kupata watalii wengi
zaidi”alisema Chambulo.
Post a Comment