Ujumbe wa Tanzania katika mkutano na Benki ya Dunia.
Kutoka
kushoto Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile,
Mkurugenzi wa Utafiti na Sera za Uchumi wa BOT Dkt. Joseph Masawe na
Naibu Gavana wa BOT Bi. Natu Mwamba wakitafakari kwa makini majadiliano
hayo.
Bw. Shahid Yusuf ambaye ni Consultant wa AFCE akichangia hoja katika mkutano wa ujumbe wa Tanzania na Benki ya Dunia.
Bw.
Paul Brenton Trade Practice Leader- AFTPM akitoa ufafanuzi pembeni yake
ni Bw. Danny Leipziger – aliyekuwa Mkuu wa Idara ya kupunguza umasikini
na kuinua uchumi.
Bw.
Zenfack, katikati akifafanua jambo katika mkutano huo, kulia ni Bw.
Philippe Dongier Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda,
Uganda na Burundi.(Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma – Washington DC).
Ujumbe
wa Tanzania wakutana na Benki ya Dunia mjini Washington DC na kufanya
majadiliano juu ya usimammizi wa uchumi wa Tanzania. Akizungumza katika
mahojiano hayo, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile
alisema kuwa kikubwa kilichojadiliwa katika majadiliano hayo ni
masuala ya ajira kwa vijana na wanawake.
‘Katika
suala zima la ajira tumeangalia ni namna gani tunaweza kuzalisha ajira
zaidi na ni sekta zipi ambazo ni muhimu, na ambazo tunaweza
kuziangalia. Suala la kilimo ndio hasa limeonekana kuwa na tija zaidi
kwa sababu kilimo kinachukua watu wengi sana kwa Tanzania.’ Alisema
Likwelile.
Katika
mazungumzo hayo ujumbe kutoka Tanzania uliweza kujadiliana na Benki ya
Dunia kuhusiana na miundombinu hasa barabara, masuala mazima ya
upatikanaji wa umeme pamoja na masuala ya bandari.
Katika
mazungumzo hayo walijikita zaidi katika sekta zisizo rasmi ambapo
ndiko kuna watu wengi na wamekubaliana kuwa wataangalia ni namna gani
tija inaweza kuimarishwa na masuala mazima ya ajira, elimu na ujuzi wa
watu kuweza kufanya kazi.
Katika
kuhitimisha majadiliano hayo Dkt. Likwelile alisema kuwa Benki ya Dunia
wanakamilisha ripoti kwa kushirikiana na tume ya mipango ili baadae
tuwe na vitu ambavyo vitasaidia katika sera zetu na suala zima la ajira
na uchumi mzima unaweza kuangaliwa.
Mikutano hii ya mwaka bado inaendelea hapa mjini Washington DC.
Post a Comment