
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kindondoni, Bi. Florence Masunga akihutubia kwenye mkutano wa UWT ulifanyika Octoba 19-2013 kwenye Kituo cha Mabasi ya Daladala cha Mwenge jijini Dar se Salaam lengo ni kuwahamasisha wanawake nchini kudumisha upendo na amani na kujiletea maendeleo. 

Katibu wa wa UWT Wilaya ya Kindondoni, Bi. Huba Issa akihutubia katika mkatano huo
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akitoa neno kwa wanachama wa
CCM na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Salum Madenge akitoa neno kwa wanachama wa
CCM na wananchi waliohudhuria kwenye mkutano huo. 
Msanii wa Kundi la Taarab la Five Star, Siwai akiimba kwenye mkutano huo.
Wanachama
na viongozi wa CCM wakiwa kwenye picha ya pamoja, (mwenye pensi nyeupe)
ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mwenge, Bw. Kessy Tuyuyu.
Wanachama wa UWT na wananchi wa kawaida wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida,akiwaonyesha wanachama
wa CCM kadi ya CHADEMA mara baada ya kukabidhiwa.
Wanachama wapya wakila kiapo,(wa pili kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akiwaongoza wanachama katika zoezi hilo.
Wanachama
na viongozi wa CCM wakiwa kwenye picha ya pamoja, (mwenye pensi nyeupe)
ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mwenge, Bw. Kessy Tuyuyu.
Wanachama wa UWT na wananchi wa kawaida wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida,akiwaonyesha wanachama
wa CCM kadi ya CHADEMA mara baada ya kukabidhiwa.
Wanachama wapya wakila kiapo,(wa pili kushoto) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akiwaongoza wanachama katika zoezi hilo.
Picha, Habari na Philemon Solomon wa fullshangwe Dar es Salaam
Umoja wa Wanawake (UWT) Kata ya Kijitonyama, jijini Dar es Salaam
umetoa rai kwa wanawake kote nchini kujitokeza kwa wingi kwenye chaguzi
mbalimbali ili Chama cha Mapinduzi kiendelee kuongoza nchi.
Rai
hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa umoja huo Wilaya ya Kinondoni, Bi.
Florence Masunga kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kituo cha Mabasi
ya Daladala cha Mwenge jijini Dar se Salaam uliokuwa na lengo la
kuwahamasisha wanawake nchini kudumisha upendo na amani na kujiletea
maendeleo.
Masunga
alitoa kauli hiyo wakati akijiandaa kumkaribisha mgeni rasmi wa mkutano
huo, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida
ambapo alisema wanawake ndiyo wanaoweza kuifanya CCM kuendelea kuongoza.
“Nawaomba
wanawake mjitokeze kwa wingi katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa
na uchaguzi mkuu kuliko ilivyokuwa huko nyuma,” alisema Masunga.
Naye
Katibu wa UWT Wilaya ya Kinondoni, Huba Issa alikisifia Chama Cha
Mapinduzi kwamba ndicho pekee kinachopaswa kuongoza nchi na siyo vyama
vya upinzani.
Katibu
huyo aliongeza kwamba kama Watanzania wanataka kuendelea kuishi kwa
amani hawana budi kuachana na wapinzani ambao hawana sera nzuri kama za
CCM.
Naye
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Bw. Salumu Madenge akizungumza
kwenye mkutano huo alisisiza Watanzania kuzidi kukichagua Chama Cha
Mapinduzi kwa sababu kina sera nzuri na ndicho kilicholeta maendeleo
yanayoonekana.
“CCM
imejenga shule, barabara, hospitali ambapo hivi sasa tunasafiri kutoka
Feri hadi Mwanza kwa kupita kwenye lami zinazoteleza…inashangaza sana
unapomuona mtu anaibuka na kusema CCM haijafanya kitu chochote,” alisema
Madenge.
Baada
ya kumkaribishara mgeni rasmi, Madabida, naye kama wenzake
waliomtangulia alisisitiza wananchi kuendelea kukichagua Chama cha
Mapinduzi ili kiendelee kuongoza nchi.
“Jamani
kila mtu anayaona mambo yaliyofanywa na CCM kuanzia awamu ya kwanza ya
Mwalimu Nyerere ambaye alijenga umoja na mshikamano wa kitaifa na msingi
wa amani, awamu ya pili ya Rais Mwinyi alitoa ukilitimba na kuleta
mfumo wa uchumi uria,” alisema Madabida na kuongeza:
“Awamu
ya tatu ya Rais Mkapa alileta uchumi wa kisasa wa kujitegemea na awamu
ya nne imeleta kasi ya maendeleo ya watu na nchi kwa ujumla.”
Katika
mkutano huo, kijana Rashid Shabaan aliyekuwa mwanachama wa Chadema,
aliachana na chama hicho na kujiunga na CCM, pia wanawake kadhaa
walikabidhiwa kadi za CCM baada ya kujiunga na chama hicho ambapo
walikula kiapo cha utii.
Kabla
ya kufanyika kwa mkutano huo, lilifunguliwa tawi la UWT la Ally Maua.
Mkutano huo ulihudhuriwa pia na baadhi ya wanachama wa CCM kutoka
Zanzibar na ulipambwa na burudani za muziki.


Post a Comment