Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Vigogo sasa wahamisha mabilioni Uswisi

 

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe
MABILIONI ya fedha za Watanzania yanayodaiwa kufichwa katika Benki mbalimbali za mataifa ya Ulaya, yameanza kufichwa. Taarifa za kufichwa kwa mabilioni hayo, zimetolewa kwa gazeti hili na mmoja wa mawaziri waandamizi wa Serikali ambaye hata hivyo aliomba kwa kusisitiza jina lake lisitajwe kwa sasa kwa sababu hatua hiyo inaweza kuharibu mwenendo wa uchunguzi wa sakata hilo wa jopo la wataalamu lililoundwa na Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni na Maendeleo (Eurodad).

Akizungumza kwa njia ya simu na gazeti hili jana, waziri huyo alisema viongozi wa Serikali, wanasiasa na wafanyabiashara waliotoroshea fedha katika benki za nje, wamepatwa na wasiwasi baada ya kusikia kuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, ameteuliwa kwenye jopo hilo.

Alisema hofu hiyo inasababishwa na jinsi Zitto alivyo na taarifa nyingi za wanasiasa na viongozi wa Serikali walioficha fedha nje, ambazo zitalisaidia jopo hilo kufanya uchunguzi wake kwa ufanisi.

Waziri huyo alisema tayari baadhi ya vigogo wamekwishatuma wakala wao katika benki walizohifadhi fedha zao nje ya nchi, ili kuangalia namna ya kuzihamisha au kubadili majina ya umiliki wa akaunti zao.

Alipoulizwa iwapo taarifa hizi zimekwishalifikia jopo la uchunguzi na hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa na jopo hilo ili kukabiliana na jambo hilo, alisema anaamini kuwa jopo hilo lina watu wenye utaalamu wa kutosha wa masuala ya kifedha, hivyo jitihada za kuficha ukweli unaofanywa sasa na watu wanaotuhumiwa hazitafanikiwa.

“Hili suala la Zitto kuteuliwa kwenye jopo la wataalamu wa Eurodad si la hivi karibuni, lina muda kidogo, tayari walengwa walishapata taarifa hizo na kuamua kufanya harakati za kuziondoa fedha zao ama kubadilisha majina kwenye akaunti zao za nje ili kujiweka salama, maana kama unavyojua kijana huyu hana hongo katika mambo yanayohusu maslahi ya taifa.

“Hili ni moja ya masuala ya kitaifa, lazima atawaumbua akiwabaini na hilo ndilo walengwa hawalitaki, wanaogopa na ndio sababu ya kutafuta legitimacy (uhalali) wa kuendelea kuyamiliki mabilioni yao,” alisema waziri huyo.

Taarifa hizi zimevuja wakati tayari Zitto yuko Geneva, Uswisi alikokwenda kuungana na jopo la uchunguzi kwa ajili ya kazi hiyo.

Uchunguzi huo utamfanya Zitto kwenda katika nchi za Ujerumani, Ubeljigi na Norway na kisha atatakiwa kuandika ripoti maalumu itakayokuwa na mapendekezo ya kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika atakayoiwasilisha kwenye mtandao unaoshirikisha Mashirika yasiyo ya kiserikali yapatayo 48 kutoka mataifa 19 ya Ulaya.

Mbali na jukumu hilo linalomkabili akiwa nje ya nchi, pia atakwenda Uingereza ambako amealikwa kutoa mada inayohusu masuala ya kodi za kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government Partnership), kabla ya kukutana na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Uingereza.

Zitto ndiye aliyeibua kwa mara ya kwanza sakata la utoroshaji fedha za umma nje ya nchi akiwa bungeni mjini Dodoma, ambapo Mwaka 2012 aliwasilisha hoja binafsi ambayo ililisaidia Bunge kupitisha azimio la kutaka uchunguzi ufanyike.

Bunge liliunda kikosi kazi cha azimio hilo kinachotarajiwa kuwasilisha taarifa yake katika Mkutano wa 16 wa Bunge, ambao unatarajiwa kuanza wiki ijayo, mjini Dodoma.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top