Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa IringaNdugu Jesca Msambatavangu akiwaongoza viongozi wa
vyama vya ukombozi mara tu walipowasili mkoani Iringa kwa ziara ya siku
moja ya kutembelea chuo cha Ihemi, Viongozi hao wapo nchini kuhudhuria
mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vya Ukombozi utakaofanyika
tarehe 9,Septemba 2013 jijini Dar es salaam.
Viongozi
mbalimbali kutoka vyama vya ukombozi wakifurahia ngoma za asili wakati
walipowasili kwenye uwanja wa ndege wa nduli tayari kwa ziara ya siku
moja kukitembelea chuo cha Ihemi.
Viongozi
kutoka vyama vya Ukombozi Afrika wakionyesha ishara ya mshikamano
wakati Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwakaribisha rasmi
kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa.
Katibu
Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa
kuwakaribisha viongozi wa Vyama vya Ukombozi katika chuo cha Ihemi.
Viongozi
kutoka vyama mbali mbali vya ukombozi Afrika pamoja na marafiki wa
vyama hivyo kutoka China wakiangalia eneo la Chuo cha Ihemi
walipotembelea leo mkoani Iringa.
Katibu
Mkuu wa Chama cha SWAPO Ndugu Nangolo Mbumba akizungumza na waandishi
wa habari baada ya kutembelea eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana
kitajengwa na kusema Tanzania ni nchi ambayo imefanya kazi kubwa
kulikomboa bara la Afrika.
Sehemu ya eneo la chuo cha Ihemi mkoani Iringa ambapo kitakapojengwa chuo kikubwa cha Uongozi kwa Vijana.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Katibu Mkuu wa chama cha
Flerimo cha Msumbiji Ndugu Filipe Paumda pamoja na wageni wengine kutoka
vyama vya ukombozi Afrika na chama rafiki cha kikomunisti cha China
wakitembelea maeneo mbali mbali kwenye chuo cha Ihemi ambapo kitajengwa
chuo cha Viongozi Vijana .
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi akiwaonyesha viongozi kutoka vyama vya
Ukombozi Afrika ,ukubwa na uzuri wa eneo ambalo chuo cha Viongozi Vijana
Afrika kitajengwa.
Mratibu
wa Chuo cha Ihemi Ndugu Lucas Kisasa akifafanua baadhi ya mambo muhimu
ya chuo hicho kwa Naibu Waziri katika Idara ya Kimataifa kutoka china
Ndugu Ai Ping .
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akizungmza na Billy
Masetlha na Obed Bapela kutoka chama cha ANC cha Afrika Kusini wakati wa
ziara yao kwenye chuo cha Ihemi mkoani Iringa.
Viongozi
mbali mbali wa vyama vya Ukombozi wakiagana na viongozi wa CCM mkoa wa
Iringa baada ya kukamilisha ziara yao ya siku moja ya kutembelea chuo
cha Ihemi mkoani hapo.
Post a Comment