Picha juu mmoha kati ya watuhumiwa akionyesha Kiganja hicho kilihifadhiwa ndani ya chungu na picha ya chini kiganja chenyewe
Watuhumiwa wakiwa na kiganja hicho cha binadamu.
Ulinzi uliimarishwa katika eneo hili kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa.
Wananchi wakiwa katika hali ya kutafakari juu ya tukio hilo la kusisimua.Picha Zote na Habari na Mdau Gsengo
---
WAGANGA
wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja, wamenaswa jijini Mwanza,
wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu.
Watuhumiwa
hao waalikamatwa jana mchana majira ya saa 9 katika eneo la Ziwani na
Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi
la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na hatimaye kufanikiwa.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo, akitihibitisha tukio
hilo, alisema kwamba mkono huo uliokuwa umewekwaa kwenye begi na ambamo
ulikuwa umefungwa kwenye kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na
kuviringishwa kwenye kalatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Konyo
ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO),
alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka
36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Alisema
kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka
mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa
watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia wanunuzi (polisi) kuwa
wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu
endapo wangezihitaji.
“Taarifa
hizi ni za awali maana tukio lenyewe bado ni bichi kabisa na limetokea
muda mfupi uliopita hivyo taarifa zaidi tutazitoa baada ya kukukamilisha
upelelezi wetu ikiwa pamoja na kuwakamata watuhumiwa na kubaini
binaadamu aliyeuawa na kukatwa baadhi ya viungo ambavyo waganga hao
walidai wanaweza kuvipata.” Alieleza.
Kamanda
Konyo pamoja na kuwapongeza wananchi waliotoa taarifa zilizofanikisha
mtego huo, alisema jeshi lake liko katika harakati za kupambana na
mauaji na uhalifu wa kila aambapo tayari kikosi kazi kiko katika wilaya
ya Magu kikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kinawatia
mbaroni watu wanaojihusisha na uhalifu na mauaji.
Credit: GSENGO
Post a Comment