Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WANANCHI WA MWENGE NYUMA YA MAGHROFA YA JWTZ WAAMUA KUJITOA MUHANGA NA KUSHIKA KINYESI KUZIBUA CHEMBA ZA MAJI TAKA, DAWASCO WAFIKA KWA KUCHELEWA.

 


Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate  kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita
Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua
Hali ni Tete eneo Hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo  maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka.
Ilikuwa ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia wenyewe,hatimaye  walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
 Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top