Waziri
wa Nchi,Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina
Kombani (wa pili kulia) akishiriki kuimba wimbo wa umoja wa wafanyakazi
muda mfupi kabla ya kufungua kikao cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa
chuo cha watumishi wa umma Tanzania.Wa kwanza kulia ni Kaimu mkuu wa
mkoa wa Singida, mwalimu Queen Mlozi.
Baadhi
ya watumishi wa chuo cha Utumishi wa Umma wakishiriki kuimba wimbo wa
umoja wa wafanyakazi muda mfupi babla ya kikao cha 16 cha baraza la
wafanyakazi wa chuo cha watumishi wa umma Tanzania kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Katala Beach mjini Singida.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina
Kombani, akizungumza katika ufunguzi wa kikao cha 16 cha baraza la
wafanyakazi wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania kilichofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Katala Beach Singida mjini.Kulia ni kaimu mkuu wa
mkoa wa Singida,mwalimu Queen Mlozi na kushoto ni mkuu wa chuo cha
utumishi wa umma Tanzania na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi, Saidi
Nassoro.
Baadhi
ya wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa chuo cha utumishi wa umma,
wakisikiliza kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye kikao cha 16
cha baraza la wafanyaka kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa
Katala Beach mjini Singida.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina
Kombani (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa kikao
cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania.
Wa watatu kulia ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na mkuu wa wilaya ya
Singida, mwalimu Queen Mlozi.Wa kwanza kulia ni afisa sekratieti
serikali za mitaa Willbord Marandu na anayefuata ni mwenyekiti wa TUGHE
taifa Dk.Diwani Mrutu.Wa tatu kushoto ni mkuu wa chuo cha utumishi wa
umma Tanzania na mwenyekiti wa baraza la wafanyakazi,Saidi
Nassoro.(Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais na Menejimenti ya Utumishi wa Umma,Celina
Kombani,amekiangiza chuo cha utumishi wa umma na taasisi zake
zihakikishe ushirikishwaji wa watumishi katika kufanya maamuzi muhimu
mahala pa kazi unapewa nafasi.
Amesema
ushirikishwaji huo utaongeza ufuatiliaji wa utekelezaji wa maamuzi
yanayofanywa, ili kuongeza mafanikio na maendeleo ya taasisi husika,
ikiwemo chuo cha utumishi wa umma.
Waziri
Kombani ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye ufunguzi wa kikao
cha 16 cha baraza la wafanyakazi wa chuo cha watumishi wa umma Tanzania
kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Katala beach mjini Singida.
Akifafanua
zaidi,waziri Kombani amesema ushirikishwaji huo utaongeza uzalishaji,
kuimarika kwa nidhamu, uwajibikaji, kukomaa kwa demokrasia mahali pa
kazi na kujenga mahusiano bora kazini.
“Pia
ushirikishwaji huu wa watumishi katika kufanya maamuzi muhimu mahali pa
kazi,utasaidia kujenga maadili ya watumishi wa umma na kutoa huduma
bora kwa wateja na wadau wa chuo pamoja na kuboresha maslahi ya
watumishi”,amesema.
Aidha,
Kombani amesema ushirikishwaji wa watumishi katika maamuzi mbalimbali
ya kiuongozi, utumike katika kijizatiti na kutatua changamoto za taasisi
husika na kuongeza uwajibikaji katika kuhudumia umma wa Watanzania kwa
unyenyekevu.
“Napenda
kusisitiza kwamba tija na ufanisi, ndiyo viwe vigezo na vipimo vya
kwanza vya vikao vya mabaraza, vitapelekea kuangalia maboresho ya
maslahi ya watumishi. Kwani uzalishaji duni utasaidia maslahi kwa
watumishi”,amesema.
Kombani
alitumia fursa hiyo kuwahimiza na kuwaasa waajiri wakitumie chuo cha
utumishi wa umma Tanzania kupata mafunzo muhimu kwa waajiriwa wao.
“Mafunzo
elekezi kwa waajiriwa wapya yatolewayo na chuo chetu cha utumishi ni
muhimu mno ili kuweza kuongeza ufanisi katika taasisi za umma na
kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa Watanzania”,alifafanua Waziri
Kombani.
Post a Comment