Na Abdi Suleiman, Pemba.
WATU 18, wamenusurika kufa akiwemo Sheha wa shehia ya Kilindi Abou
Abrahman Salum (67) huku majeruhi Tisa (9) wakilazwa hospitalini, baada
ya gari waliyokuwa wamepanda kuanguka huko katika barabara ya Tundauwa
Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Majeruhi waliopata ajali hiyo wakifikishwa katika hospitali ya Chake Chake Pemba
Tukio hilo lililotokea majira ya saa moja na robo (1:15) za asubuhi ya
leo, wakati gari hiyo iliyokuwa ikitokea Tundauwa kwelekea mjini Chake
Chake, iliposhindwa kupanda kilima cha Kunguni na kurudi nyuma na
kuanguka.
Majeruhi waliopokelewa katika hospitali ya Chake Chake, ambao
wamenusurika kifo ni pamoja na Salum Mohamed Salum (70), Haji Salum
Mohamed (23), Mzee Juma Saburi (50), Siti Massoud Dadi (60), Saidi Seif
Nassor (23).
Wengine ni Ameir Khatib (19), Suleiman Ramadhan Aboud (23), Mariyam
Khamis (32), Abdalla Suleiman Abrahman (30), Zubeda Faki (38), Fatma
Abeid Khamis (36), Amina Mohamed Abeid (40) na Abou Abrahman Salum (67),
wote ni wakaazi wa Kilindi.
Majeruhi wengine ni Fatma Ali Juma (70),
Fatma Khamis Ali wakaazi wa shengejuu, Nassor Abdalla Nassor (50) mkaazi
wa Kungeni na Rajab Ali Juma (43) mkaazi wa Tundauwa.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kanda wa Polisi Mkoa wa Kusini
Pemba, Saleh Mohamed Saleh alisema kuwa, gari hiyo iyopata ajali ilikuwa
ikiendeshwa na dereva Ali Salum Suleiman (25) mkaazi wa Tundauwa.
Kamanda Saleh aliitaja gari hiyo yenye No Z884 BE yenyeruti Kilindi
Chake, ilishindwa kupanda kilima cha Kunguni na kurudi nyuma na
kupinduka, huku dereva akishikiliwa na polisi.
Aidha alisema kuwa, katika majeruhi hao Tisa mmoja kati yao Mzee Juma
Saburi, amepelekwa Hospitali ya Mkoani kwa matibabu zaidi baada ya
kuumia mguu.
“Ajali imetokea kweli, bahati nzuri hakuna mtu aliyepoteza maisha, ila
majeruhi walichunika chunika kidogo katika sehemu za kichwani, mikononi
na kutibiwa na kuruhusiwa kwenda zao majumbani”alisema kamanda Saleh.
Hata hivyo aliwataka madereva kuwa na tahadhari sana wakati
wanapoendesha gari zao, kwa kuziangalia kabla ya kuanza safari, ili
kuweza kuepuka ajili zisizokuwa za lazima.
Via ZanziNews


Post a Comment