Na Eliphace Marwa – MAELEZO
Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi anatarajia kufungua mkutano
wa siku mbili wa Maafisa waandamizi wa Jeshi la Magereza utakaofanyika
kuanzia Oktoba 24, mwaka huu mkoani Morogoro.
Mkutano huo
ndiyo mkutano wa juu kabisa katika jeshi la Magereza ambao uwahusisha
wakuu wa Magereza wa Mikoa ya kiutawala Nchini, Maafisa waandamizi toka
Makao Makuu pamoja na Wakuu wa Taasisi sita za ndani ya jeshi la
Magereza ambazo kimuundo wa utawala zina hadhi ya mikoa.
Taasisi hizo
ni pamoja na Chuo cha maafisa Ukonga mkoani Dar es Salaam, Chuo cha
mafunzo ya awali Kiwira Mkoani Mbeya, chuo cha Ufundi Ruanda Mbeya, chuo
cha Udereva na ufundi mitambo cha Kingilwira mkoani morogoro, kikosi
Maalum cha kutuliza ghasia Magerezani Ukonga Dar es Salaam pamoja na
Shule ya Sekondari Bwawani iliyoko mkoani Pwani.
Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Juma Mlewa kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, John
Casmir Minja inasema kuwa madhumuni ya mkutano huo wa kila mwaka ni
kutathmini kwa pamoja utendaji wa jeshi hilo katika maeneo yake yote na
kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizopo pamoja na
kurekebisha dosari zilizojitokeza na kuweka malengo ya kuboresha
utendaji kazi katika mwaka unaofuata.
Mkutano huo,
ambao mada kuu itakuwa ni utendaji kazi wa kasi na tija kwa matokeo
makubwa sasa pia watazungumzia fursa mbalimbali za kuwezesha jeshi hilo
kujitegemea, mpango wa uchangiaji wa hiari Mfuko wa Pensheni kwa
Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na mada ya urekebishaji wafungwa
itakayotolewa na Makao makuu ya Magereza.
Mkutano huo unatarajiwa kufungwa na kamishna Jenerali wa Magereza John Minja.



Post a Comment