Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WENGI WAJITOKEZA KUMZIKA JAMES KOMBE MKOANI KILIMANJARO

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT,
kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao akiendesha Ibada ya Maziko
ya  aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyefariki dunia Oktoba 21
mwaka huu, Jijini Dar es salaam na Kuzikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji
cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi
Vijijini,
mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama akitoa heshima za
mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama
Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mkuu wa wilaya ya Hai, Novatus Makunga (wakwanza) na Mkuu
waWilaya ya Moshi, Dkt. Ibrahimu Msengi (wa pili) wakitoa heshima zao
za mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama
Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Kamanda
wa Polisi mkoanbi Kilimanjaro, ACP-Robert Boaz akitoa Salamu za
Rambirambi kwa niaba IGP Said Mwema katika ibada ya Maziko ya aliyekuwa
Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi wa Polisi,
James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani kwake, kijiji cha Msae, Kata ya
Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini,
mkoani Kilimanjaro.
Mheshimiwa Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Moshi, Mkoani
Kilimanjaro, Aisha Nyerere, akitoa heshima za mwisho katika Jeneza la
aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mke wa Marehemu, Maria Kombe (katikati) pamoja na watoto wake
wakifuatilia ibada ya Maziko ya Mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo
cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama (katikati),
Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz (kulia) na Kaimu
kamanda wapolisi mkoani Kilimanjaro, Moita Koka, wakitoa heshima za
mwisho katika Jeneza la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama
Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mwili wa aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, ukiondolewa kanisani katika
kanisa la KKKT, usharika wa Msae kuelekea Nyumbani kwake kwa ajili ya
zoezi ya Maziko yaliyofanyika Jana, kijijini Msae, kata ya Mwika,
wilaya ya Moshi Vijijini, Mkoani Kilimanjaro.
Askofu Mkuu wa KKKT kanda ya Kaskazini, Dkt. Martin Shao,
akiweka Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama
Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini,
mkoani Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, akiweka Ua katika
Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini,
mkoani Kilimanjaro.
Kamanda wa Polisi kilimanjaro, Robert Boaz na Kamanda wa
Polisi Arusha, Liberatus Sabas (mwenye suti) wakiweka
Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Mke wa Marehemu, Maria Kombe, akiweka
Ua katika Kaburi la Marehemu mume wake, aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha
Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Wanafamilia wakiweka
Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Watoto wa Marehemu Kombe, wakiongozwa na Kaka yao, Dustan
Kombe kuweka  Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha
Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
 
Jaji wa Mahakama
Kuu kanda ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Aisha Nyerere,

akiweka
Ua katika Kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, aliyezikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro.
Vijana wa Jeshi la Polisi, wakitoa Heshima za mwisho katika
kaburi la aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama Barabarani,
Kamishna Msaidizi wa Polisi, James Kombe, kwa Mujibu waTaratibu
zaKijeshi. Kombe alizikwa Jana Nyumbani
kwake, kijiji cha Msae, Kata ya Mwika, wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani
Kilimanjaro. picha zote na Taifa Letu.com blog
Na Mwandishi Wetu,
Kilimanjaro
 
MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, amewaongoza Maelfu
ya
waombolezaji katika mazishi ya Aliyekuwa Mkuu wa kitengo cha Usalama
Barabarani, Kamishna mstaafu, James Kombe (63), aliyefariki dunia
October 21 mwaka huu katika Hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es
salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kombe aliyeitumikia Jeshi la Polisi kwa muda wa miaka 24, katika
nyadhifa mbalimbali, alizikwa jana saa 9:40, alasiri, Nyumbani kwake
katika kijiji cha Msae, kata ya Mwika, Jimbo la Vunjo, wilaya ya Moshi
vijijini, mkoani Kilimanjaro baada ya ibada ya maziko iliyofanyika
katika Usharika wa Msae-Lyakrima na kuongozwa na Askofu Mkuu wa KKKT,
dayosisi ya Kaskazini, Dkt. Martin F. Shao.
Akitoa Salamu za Rambirambi, Gama alisema serikali imeguswa na msiba
huo huku akimuelezea Marehemu Kombe kama mtu muadilifu, mwaminifu na
mtu asiyekuwa, asiyekuwa na ubinafsi na mzalendo aliyeitumikia Taifa
lake kwa nguvu zake zote hadi dakika za mwisho za uhai wake.
“Ni kweli mazingira yetu kikazi yanatofautiana, lakini ni wazi kuwa
kuna mengi ya kujifunza na kujivunia kutoka kwa Kamishna Kombe enzi za
uhai wake, Marehemu ameacha historia iliyotukuka nyuma yake, alikuwa
ni mtu mwadilifu sana, mwaminifu, mzalendo na mchapa kazi
aliyejitoleakulitumikia Jeshi la Polisi na Taifa kwa ujumla,” alisema
Gama.
Kuhusu swala la uwajibikaji na utendaji kazi, Gama alisema wananchi
wengi kwa sasa wanashindwa kufanya kazi za maendeleo hasa mkoani
Kilimanjaro katika maeneo ya Rombo, Marangu na Mwika kutokana na
kukithiri kwa vitendo vya Unywaji pombe holela ambapo aliagiza wakuu
wa wilaya kuhakikisha wanasimamia na kudhibiti hali hiyo.
Awali akiongoza Ibada ya Maziko, Askofu MKuu wa KKKT, dayosisi ya
Kaskazini, Dkt.
Martin Shao, aliwataka waumini wa dini ya Kikristo, wananchi pamoja na
watumishi katika Jeshi la Polisi kufanya yale yaliomema ikiwa kweli
wanataka kuenziwa kama ilivyo kwa Marehemu Kombe.
Dkt. Shao katika ibada hiyo alimuelezea Marehemu Kombe kama mtu
anayestahili kuenziwa daima kama anavyoenziwa Hayati Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka na utendaji wake kazi
uliotukuka, uzalendo na Uadilifu pamoja na uwajibikaji katika
kuhakikisha Amani ya Tanzania na usalama wa Wananchi wake.
Kabla ya kifo chake, Kamishna Kombe, alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa
wa Kansa ambao ulianza kumsumbua Juni mwaka jana na kutibiwakatika
Hospitali ya Rufaa KCMC mjini Moshi.
James Kombe, aliyezaliwa mwaka 1950, mwika Kilimanjaro ameacha mjane
mmoja, Maria Kombe na watoto watano na kwamba alilitumikia Jeshi la
polisi kuanzia Machi, mwaka 1970 na kulitumikia mpaka alipostaafu
mwaka 2010.
Akisoma historia ya Marehemu, Kamanda wa kikosi cha usalama
Barabarani, Joseph Mwakabonga alisema Kamishna Kombe, alijiunga na
Mafunzo ya awali machi 23 mwaka 70 na kumaliza Agosti 28 mwaka huo,
huko Mopshi baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini
Uganda.
Alisema alipandishwa vyeo kama Mkaguzi wa polisi (1977), Kamishna
msaidizi (1995), Mkaguzi wa polisi (1986), mrakibu mwandamizi (1991)
na Kamishna Msaidizi wa Polisi (2002) hadi alipostaafu
2010.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top