Serikali Kikwazo
Wakati
shinikizo la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na
Utoroshaji wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania
inavuta miguu.
Moja
ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni makubwa
ya kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa
(automatic exchange of tax information) .
Kufutia
shinikizo la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy
jurisdictions" (tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa
taarifa. Tanzania mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa
taarifa yeyote kwa Umma.
Ghana,
Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama
Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za
kigeni nchini zinatokana na mauzo ya madini nje. Makampuni ya madini
ndio yanaongoza kukwepa kodi.
Tanzania
inapoteza jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni
1.25 kwa mwaka kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi.
Hii ni sawa na kusema Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili
kila siku kwa uporaji huu.
Naitaka
serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa
mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania
inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa
kuvuta miguu katika suala nyeti la umma. Badala ya kukimbilia kutoza
kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa yanayonyonya rasilimali
zetu yanalipa kodi inayotakiwa.
Zitto Kabwe, MB
Waziri Kivuli wa Fedha
24 Oktoba, 2013
Geneva, Switzerland
Post a Comment