
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe
kuashiria uzinduzi wa mradi wa vijana waendesha pikipiki mjini Mbinga
ambao unafadhiliwa na mbunge wa jimbo la Mbinga Mh Gaudence Kayombo,
uzinduzi huo umefanyika kwenye mkutano wa hadhara ulioafnyika kwenye
uwanja wa Taifa mjini Mbinga, Kinana yuko katika ziara ya mikoa mitatu
Ruvuma, Mbeya na Njombe akiongozana na Dr.Asha
Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kiamataifa na Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi. akikagua miradi ya
maendeleo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ikiwani
pamoja na kuimarisha uhai wa chama, Kushoto ni Mbunge wa jimbo la
Mbinga Gaudence Kayombo na kulia ni Mwenyekiti wa kikundi cha waendesha pikipiki wa Mbinga Al Haji Mussa Ramadhan(PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MBINGA)

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
mwenyekiti wa shina katika kijiji cha Amani Makolo wakati alipowasili
katika jimbo la Mbinga leo 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana wa nne kutoka
kulia akiongoza viongozi wa CCM Mkoa wa Ruvuma na Wilaya ya Mbinga
katika kilimo kwenye shamba la akina mama na vijana wa mjini Mbinga
walioanzisha umoja wao kwa kuanzisha kilimo cha alizeti wakisaidiwa na
Mbunge wao na Mkuu wa Wilaya, Shamba hilo lina ekari 500 na kwa sasa
wameshalima hekari 100 na wanaendelea na upanuzi wa kilimo katika shamba
hilo ambalo wameazimwa na Jshi la Magereza

Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wa kwanza waliovaa
mashati ya kijani akiwa amekaa na wanachama wa CCM katika kijiji cha
Amani Makolo leo. 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana kulia na Nape
Nnauye waliopanda pikipiki wakijaribu kuziwasha pikipiki hizo mara baada
ya kuzindua mradi huo wa vijana mjini Mbinga. 

Wana CCM wa Kijiji cha Amani Makolo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati akizungumza nao 

Wana CCM wapya wa Amani Makolo wakila kiapo mara baada ya kupokea kadi zao za uanachama. 

Nape Nnauye akifurahia jambo na Bibi Dafroza Luoga wakati alipokuwa wakizungumza mawili matatu na bibi huyo. 

Wananchi
wa kijiji cha Amani Makolo wakifurahia ghala lao la kuhifadhia mahindi
mara baada ya katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kukagua ghara
hilo. 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wananchi katika kijiji cha Mtunduwalo Wilayani Mbinga. 4t

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
Tarn Brereton Mtendaji mkuu wa kampuni ya TANCOAL inayomiliki mgodi wa
Makaa ya mawe wa Mangaka Wilayani Mbinga wakati alipotembelea mgodi huo
kushoto ni Gideon Nasari Mkurugenzi Mkuu wa NDC. 

Mitambo mbalimbali inayofanya kazi ya kuchimba makaa ya mawe kwenye mgodi wa Mangaka.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mgodi huo leo 

Hapa ndipo kwenye mtambo wa kusaga makaa hayo. 

Dr. Asha Rose Migiro na Nape Nnauye wakisalimia wananchi wakati msafara huo ukiwa njiani kuelekea Mbinga.

Msafara ukielekea Mbinga 

Vijana
na akina mama na vijana wa Mkwaya kata ya Kilimani wakiendelea na
shughuli za kusafisha shamba lao lililopo nje kidogo ya mji wa Mbinga,
Mtangazaji wa TBC Gerson Msigwa akishiriki katika kilimo shambani Kilimani 
Mtangazaji wa TBC Gerson Msigwa akishiriki katika kilimo shambani Kilimani 
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
vijana na akina mama wenye umoja wao wanaolima shamba hilo wakati
alipokagua shamba hilo. 

Katibu
wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa
Mbinga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa
mjini Mbinga 

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia
wananchi wa Mbinga katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja
wa Taifa mjini Mbinga


Post a Comment