Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwaasa Wanajumiya ya
Watanzania wanaoishi Seattle kukumbuka hatma ya maisha yao ya baadaye
kwa kuwekeza nyumbani.
*************************************
Watanzania waishio na kuendesha maisha yao Nchini Marekani wameawa kuwa makini katika kuutumia vyema muda wao wa maisha Nchini humo kwa kufikiria mbinu za kujiwekea mitaji itakaowajengea hatma njema hapo baadaye endapo watafikia maamuzi ya kurejea kuishi nyumbani siku zijazo.

Nasaha
hizo zimetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi wakati akizungumza na Wanachama wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi
katika Mji wa Seattle ndani ya Jimbo la Washington kwenye tafrija maalum
iliyoandaliwa na wana jumuiya hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli
ya Ramada Tukwila Mjini Seattle.
Balozi
Seif alisema wapo baadhi ya Watanzania waliobahatika kupata fursa na
nafasi nzuri za kuendesha maisha katika Mataifa mbali mbali ya nje
hasa ya ulaya lakini wengi kati yao wameishia kuwa na maisha mabovu kwa
kukosa kujiwekea misingi mizuri.
Alisema
tabia ya kuendelea na kuendekeza starehe sambamba na matumizi ya
kifahari kwa msingi wa kutaka sifa hutoa sura mbaya kwao lakini
kinachoumiza zaidi ni kile kizazi chao kinachowategemea.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaomba wana Jumuiya hiyo ya
Watanzania wanaoshi Mjini Seattle kuzingatia na kuheshimu sheria na
taratibu za nchi wanayoishi ili kulinda desturi na ukarimu walionao.
Amewapongeza
wana jumuiya hiyo ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle kwa umoja na
ushirikiano waliokuwa nao bila ya mgongano na ubaguzi wa uzawa ambao
ndio utanaowasaidia katika kuimarisha mila na silka zao.
“
Ukweli sifa tulizokuwa nazo sisi Watanzania hatufanani na wenzetu wa
mataifa mengine . Hivyo Utanzania wetu ni vyema tukauendeleza kwa
kusaidiana na ofisi za balozi zetu zilizo karibu “. Alisisitiza Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Akijibu baadhi ya maswali alioulizwa na Wanajumuiya hiyo ya
Watanzania waishio Mjini Seattle Balozi Seif aliwatoa hofu wanajumiya
hao kwa kuwaeleza kwamba Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hivi sasa
inaendelea kuwa shwari licha ya vituko vinavyotokea katika baadhi ya
wakati hasa vile vilivyokuwa vikiwatia hofu wananchi vya kumwagiwa watu
tindikali.
Alieleza
kwamba Serikali iko makini katika kuhakikisha vitendo vya uvunjaji wa
amani havipewi nafasi na tayari vyombo vya ulinzi vinaendelea na
operesheni za kuwasaka watu wenye tabia kama hizo zinayotishia maisha ya
Jamii.

Akijibu swala la operesheni kimbunga iliyowakumba watu waliokuwa
wakiishi kinyume na taratibu za uhamiaji Nchini Tanzania Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali iliamua kufanya
operesheni hiyo baada ya kugundua wahamiaji haramu ndio wanaohusika na
masuala ya ujambazi Nchini.
Alifahamisha
kwamba watu wote walioondoshwa Nchini Tanzania kupitia operesheni
Kimbunga hiyo wamebainika kutokuwa na kibali jambo ambalo ni kosa
kwa mujibu wa mfumo na taratibu za uhamiaji Kimataifa.
Hata
hivyo Balozi Seif alifafanua kwamba Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kuheshimu haki za Binaadamu haijamkataza mtu wa nchi
yoyote Duniani kuishi Tanzania endapo atazingatia sheria za Nchi
zilizopo.

“ Serikali imelazimika kuwa makini katika kulinda usalama wa wananchi
baada ya kugundua kwamba wengi wa wahamiaji haramu ndio waliokuwa
wakihusika katika masuala ya ujambazi na matukio ya hatari hapa Nchini
“. Alisema Balozi Seif.
Wakitoa
salamu zao kwa wanajumiya hao Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Waziri wa Biashara,
Viwanda na Masoko Mh. Nassor Ahmed Mazrui wamewashauri wanajumuiya hao
kuzitumia fursa za mitaji zilizopo nchini humo kwa kuanzisha miradi
Nchini Tanzania.

Mawaziri hao walisema mitaji hiyo ambayo fedha zake hazina masharti
makubwa zinaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa ajira hasa kwa vijana pamoja
na kuongeza vipato vyao vitakavyopunguza umaskini.
Walieleza
kwamba wanajumiya hayo ni vyema wakaitumia Diasfora wakielewa kwamba
Tanzania ni yao na kwame bila ya wao hakutakuwa na mgeni atakayeweza
kuweka misingi ya kuimarisha uchumi wa taifa.
Mapema
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Mjini Seattle Jimboni
Washington Nchini Marekani Nd. Yona Isimika alisema jumuiya yao
iliyoanzishwa mwaka 2008 hivi sasa ina karibu wanachama Mia Nne.

Nd. Yona alisema Jumuiya yao iliyolenga kuuendeleza Utamaduni, Mila
na Silka zao za Kitanzania iko katika mchakato wa kubadilisha katiba ili
ikidhi matihaji yao hasa wakati wanapopatwa na matatizo.
Mwenyekiti
huyo wa Jumuiya ya Watanzania waoishi Seattle Washington alipongeza
Ujumbe huo wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
kwa hatua yake ya kukutana nao ikiwa ni ugeni wa mwanzo tokea
kuanzishwa kwa jumuiya hiyo mwaka 2008.



Post a Comment