Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

CCM MUFINDI YAZIDI KUJIWEKA SAWA

               


JENGO-LA-CCM-MUFINDI_428aa.jpg
Na Francis Godwin Blog Mufindi
Makatibu wa Uchumi na Makatibu Uenezi wa Kata zote 30 za Wilaya ya Mufindi, wameshiriki semina ya siku moja mjini Mafinga. Siku ya jumamosi, Novemba 9.

Kwa mujibu wa Katibu mwenezi wa CCM, Wilaya ya Mufindi, Daud Yassin, semina hiyo, ilifunguliwa na mjumbe wa nec wa Wilaya hiyo, Marselina Mkini.
Semina hiyo iliratibiwa na Katibu Mwenezi wa Wilaya, Daud Yassin, na Katibu wa Uchumi wa Wilaya, Blastus Mgimwa. Kwa lengo la kukiimarisha chama cha mapinduzi wilayani Mufindi, kwa kukumbushana majukumu ya idara za Uenezi na Uchumi, ktk ngazi za Matawi na Kata.
Washiriki wa semina hiyo, walipewa maelekezo mbalimbali juu ya utendaji na utekelezaji wa majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya CCM, ktk kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za vitongoji, vijiji na mitaa, mwaka kesho 2014, na uchaguzi mkuu mwaka 2015.(P.T)

Viongozi hao, wamehimizwa kuzingatia majukumu yao, kuwa na mshikamano, pamoja na kuwajulisha wananchi juu ya utelezaji wa ILANI ya CCM ya 2010 - 2015 katika vitongoji, vijiji na kata. Hakuna ubishi kwamba Serikali ya CCM, imefanya mambo mengi ktk utekelezaji wa ILANI, hivyo ni lazima viongozi wa CCM, ktk maeneo yote wapaze sauti kuelezea mafanikio yote yaliyopatikana, na pia waeleze yale ambayo hayajafanyika na sababu zake.
Ili kumarisha chama ktk Wilaya ya Mufindi, Katibu mwenezi wa Wilaya, na Katibu Uchumi wa Wilaya, wametoa kadi za CCM 1500, ikiwa ni wastani wa kadi 50 kwa kila Kata, ili kuingiza wanachama wapya 1500 kwa mkupuo. Waliwaeleza washiriki wa semina hiyo, kwamba ni lengo la CCM, Wilaya ya Mufindi kuingiza wanachama wapya kwa wingi, kwani kuna watu wengi ktk Wilaya hiyo wenye nia ya kujiunga na chama cha mapinduzi.
Naye mwasisi wa CCM, ambaye pia ni Mwenyekiti msaafu wa CCM, Mzee Tasil Mgoda, aliwataka viongozi hao wa CCM, ngazi ya Kata na Wilaya kuzingatia maadili ya uongozi na kuwa wakweli katika utekelezaji wa majukumu yao. Aliwakumbusha jinsi Mwalimu Nyerere, alivyopigania umoja ktk nchi yetu, na kuhimiza usawa. Mzee Mgoda alisema bado CCM ni chama imara na kitaendelea kuwa imara ktk nchi yetu.
Akizungumza katika semina hiyo, mjumbe wa nec wa wilaya ya Mufindi, alihimiza viongozi wote wa CCM, kufanya ziara kwenye mashina na matawi, kwani huko ndiko walipo wanachama wa CCM, aliwakumbusha viongozi hao kwamba, chama ni vikao na wanachama, hivyo ni muhimu sana kuwafuata wanachama kwenye matawi na mashina, ili kusikiliza kero zao, maoni yao na ushauri juu ya chama chao.
Kwa ujumla semina hiyo ilikuwa na mwitikio mzuri sana, wajumbe waliahidi kwenda kutekeleza yote waliyoelekezwa.
Wilaya ya Mufindi ina jumla ya kata 30, ambazo zote madiwani wake ni wa CCM, na majimbo mawili, ambapo pia Wabunge wake ni wa CCM.
Pia katika semina hiyo alikuwapo katibu wa CCM Wilaya hiyo ya Mufindi, Jacob Nkomola, ambaye aliwaeleza wajumbe kwamba, semina hiyo ni mwanzo tu wa mfululizo wa semina nyingi za mafunzo, zitakazo fuata.
Nkomola alisisitiza kwamba, ni lazima kila kiongozi wa ngazi husika, azingatie kutimiza wajibu wake, ili chama cha mapinduzi kiendelee kuwa imara wakati wote. Aliwataka viongozi na wanachama kuwa kitu kimoja, na vilevile, wajipange vyema wakati tukielekea kwenye uchaguzi wa mwaka kesho, 2014, na pia uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Katibu huyo wa Wilaya, pia alisisitiza umuhimu wa kubuni miradi ya chama, ili chama kiweze kuwa na uchumi mzuri, na kuweza kumudu kutimiza malengo yake. Aliwashukuru wajumbe wote kwa kuhudhuria mafunzo hayo, aliwataka kujiandaa kwa kupewa mafunzo zaidi, ili shughuli za chama ziweze kufanyika kwa ufasaha zaidi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top