LONDON, Uingereza
TANZANIA imeendelea kutengwa na wanachama wenzake wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo safari hii haijashirikishwa katika mkutano wa kusaini hati moja ya kusafiria.
Katika mkutano huo wa World Tourism Market unaoendelea nchini Uingereza ulihudhuriwa na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambapo mkataba huo unatarajiwa kuanza Januari mwakani.
Kwa kutumia hati moja ya kusafiria watu kutoka nchi wanachama wakiwemo wananchi na watalii watakuwa na uwezo wa kusafiri.
Hivi karibuni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta akiwa bungeni mjini Dodoma alisema Tanzania haitasubiri talaka bali yenyewe ndiyo itakayotoa kwa Kenya, Rwanda na Uganda.
Waziri Sitta alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa maswali na wabunge ambapo ilikuwa ni siku moja wakati marais Uhuru Kenyatta wa Kenya, Yoweri Museveni wa Uganda na Salva Kiir wa Sudan Kusini wakati wakisaini mkataba mwingine nchini Rwanda.
Marais hao walikuwa wanasaini mkataba huo wa usafirishaji bure wa bidhaa pamoja na maendeleo ya miundombinu kwa nchi za Afrika Mashariki.
Katika mkutano huo, unaoendelea, Uingereza Tanzania imeendelea kuwa nje ya vikao vya nchi wananchama katika kujadili mambo yanayozihusu nchi hizo hali inayoashiria viongozi wa nchi hizo wameamua kuitenga, Tanzania. JAMBOLEO

Post a Comment