Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini Meja Generali Mstaafu Ligate Sande akitoa hotuba
katika mahafali ya 9 ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI).
Mgeni
Rasmi Dk. Mwinjaka akimtunuku Cheti Mhitimu wa Stashahada ya Juu ya
Usafirishaji wa Majini (ADMT) Dilshad Murtaza kwa kupata Daraja la
Kwanza la GPA 4.5 kwenye Kozi hiyo
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utumishi Dk. Tumaini Gurumo
akimkabidhi Mgeni Rasmi zawadi aliyoandaliwa na chuo hicho.
Picha zote na Hussein Makame, Afisa Habari, Idara ya Habari (MAELEZO)
Hussein Makame, MAELEZO
CHUO cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kimejipanga
kutoa elimu ya rasilimali za baharini ikiwemo mafuta na gesi katika
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na dunia kwa ujumla.
Hayo
yamesemwa jana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DMI, Meja
Generali Mstaafu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
Ligate Sande katika mahafali ya 9 ya chuo hicho yaliyofanyika jijini Dar
es Salaam.
Mwenyekiti
huyo alisema wamefikia hatua hiyo ili kuifanya Tanzania ambayo ni nchi
iliyoko ukanda wa bahari wenye wingi wa rasilimali ya mafuta na gesi
kunufaia na rasilimali hizo.
Alisema
moja ya kigezo cha kuboresha na kusimamia rasilimali baharini na maeneo
yanayozunguka bahari ni kuwa na rasilimali watu ya kutosha na yenye
ujuzi na weledi katika mambo ya bahari.
Meja
General Mstaafu Sande alisema pamoja na kuwa na rasilimali watu ya
kutosha kunahitajika mikakati ya makusudi ili kuifanya Sekta ya bahari
iwe endelevu na yenye tija kwa Taifa.
“DMI
imejipanga katika kutoa elimu ya aina hii katika ukanda huu wa Afrika
Mashariki na kati na dunia kwa ujumla” alisema mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi wa chuo hicho ambacho ni Kituo cha Ubora (Centre of
Excellency) wa Elimu ya Bahari inayotambuliwa na Jumuiya ya Afrika
Mashariki.
Akizungumzia
changamoto zinazikikabili chuo hicho, mwenyekiti huyo alisema pamoja na
changamoto nyingine, DMI kina uhaba wa miundombinu ya madarasa na ofisi
za walimu katika kukidhi mahitaji ya ongezeko la wanafunzi wanaojiunga
na chuo hicho kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.
Akizungumzia changamoto hizo, Mgeni Rasmi kwenye Mahafali hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Dk. Shaaban Mwinjaka alisema anatambua umuhimu wa DMI na changamoto zinazokikabili.
“Hata
hivyo ninatambua kuwa DMI inao uwezo wa kutoa mchango wa wataalamu
katika fursa hizo hususan waendesha meli, Wahandisi wa meli, Uchimbaji
gesi na Mafuta, Usafirishaji shehena, Ukarabati wa meli, Ajira ndani na
nje ya nchi” alisema Dk Mwinjaka.
Katika mahafali hiyo yenye kauli mbiu isemayo Sekta
ya Bahari “Matokeo Makubwa Sasa” Zingatia Elimu Bora na Usawa
Kijinsia”, yalishuhudia wahitimu 403 wakitunukiwa vyeti kwa ngazi ya
Stashahada ya Juu, Stashahada na Cheti.
Mbali
na tunu hizo, wahitimu 10 walitunukiwa vyeti kutokana na kufanya vizuri
kwenye masomo katika mwaka wa masomo wa 2011/2012 na 2012/2013 akiwemo
Dilshad Murtaza aliyepata Daraja la Kwanza la ufaulu wa GPA ya 4.5
katika Shahada ya Juu ya Usafirishaji wa Majini (ADMT).
Post a Comment