TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.11. 2013.
WILAYA YA RUNGWE – AJALI YA GARI KUPINDUKA NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO
TAREHE 01.11.2013 MAJIRA YA SAA14:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI NA KATA
YA KIBOLE, TARAFA YA PAKATI BARABARA YA KIBOLE/NGYEKYE WILAYA YA
RUNGWE MKOA WA MBEYA. GARI T.628 BDL AINA YA TOYOTA CANTER LIKIENDESHWA
NA DEREVA AMBAYE HAJAFAHAMIKA JINA WALA MAKAZI YAKE LILISHINDWA KUPANDA
MLIMA NA KUPINDUKA KISHA KUSABABISHA KIFO CHA ABIRIA LUGANO S/O
MWAKALEKE, MIAKA 18, KYUSA, MWANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI SELYA KIDATO
CHA PILI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA AJALI. MWILI WA MAREHEMU
UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA KUKABIDHIWA NDUGU KWA MAZISHI. KAIMU KAMANDA WA
POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANAENDELEA KUTOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA
MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA
AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA ANATOA RAI KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA
JUU YA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE
NA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE, VINGINEVYO AJISALIMISHE MWENYEWE.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
MNAMO
TAREHE 02.11.2013 MAJIRA YA SAA 00:45HRS HUKO ENEO LA UHINDINI JIJI NA
MKOA WA MBEYA. EMANUEL S/O BASHOHO, MIAKA 17, MUHANGAZA, MKULIMA,
MKAZI WA IWAMBI ALIKAMATWA AKIWA NA NOTI BANDIA MOJA YENYE THAMANI
YA TSHS 10,000/= YENYE NAMBA BX-5273814 .MBINU NI KUKODI GARI [TAXI]
KUTOKA IWAMBI HADI UHINDINI NA KUTOA NOTI HIYO KAMA MALIPO. TARATIBU
ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA ANAENDELEA KUTOA WITO
KWA JAMII KUWA MAKINI KWA KUCHUKUA TAHADHARI KATIKA MATUMIZI YA PESA
HASA NOTI ILI KUEPUKA MATATIZO YANAYOWEZA KUEPUKIKA
[ROBERT MAYALA- ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment