 |
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) akimtambulisha Mhe. Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa
Kenya kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa
pamoja na Waandishi hao kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa hotuba
ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
aliyoitoa hivi karibuni kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Katika hotuba hiyo Mhe. Rais Kikwete alieleza msimamo wa
Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 |
| Mhe. Amina Mohammed akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huku Mhe. Membe akisikiliza. |
 |
| Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John
haule (wa pili kulia) akimsikiliza Mhe. Mohammed (hayupo pichani)
alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya
kwa Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya
Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa
Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana (wa pili kushoto) na Mjumbe
kutoka Kenya. |
 |
| Mkurugenzi
wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Dora Msechu (katikati), Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Bw. Robert Kahendaguza
(kushoto), Mjumbe kutoka Kenya na Bw. Mkumbwa Ally (mwenye koti jeusi),
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wakati wa Mkutano kati
ya Mhe. Membe na Mhe. Mohammed na Waandishi wa Habari (hawapo pichani |
|
on Monday, November 11, 2013
Post a Comment