Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (wa pili kushoto) akiongozwa na
viongozi wa Kata ya Manzese kuelekea kwenye ukaguzi wa maendeleo ya
Mradi wa Maji Safi na Salama ya Kisima katika Mtaa wa Mivuleni, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Wakazi
wa Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese, Manispaa ya Kinondoni, Dar es
Salaam wakichota maji ya mradi wa maji safi na salama ya kisima wa
Manispaa hiyo, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Kinondoni, Gonzalves Rutakyamirwa
(kushoto) akimwelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda
(mwenye shati ya drafti) maendeleo ya mradi wa Maji safi na salama ya
kisima unaotekelezwa kwenye Mtaa wa Mivuleni, Manzese, Dar es Salaam
juzi wakati Meya huyo alipofanya ziara ya ukaguzi wa miradi hiyo kwenye
Kata tisa za Manispaa hiyo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni Diwani wa
Kata hiyo, Eliam Manumbu na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya
Mipangomiji na Mazingira, Richard Chengula.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni Yusuf Mwenda (mbele kulia) akikagua kivuko
kinachounganisha Kata ya Sinza na Kijitonyama, Dar es Salaam wakati
alipofanya ziara ya ukaguzi wa Mendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa Maji safi
na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E mwishoni mwa wiki.
Mkandarasi wa Kampuni ya Drilling and Dam Construction Agency, Elzei
Makaso (kulia) akimelezea Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda
(kushoto) maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Maji safi na Salama ya Kisima
katika Mtaa wa Magomeni Dosi, Dar es Salaam wakati Meya huyo alipofanya
ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuf Mwenda (kushoto) akizindua Mradi wa
Maji safi na salama ya kisima katika Mtaa wa Sinza E, Dar es Salaam
wakati alipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo mwishoni
mwa wiki. Kushoto kwake ni Diwani wa Kata hiyo (CHADEMA), Renatus Pamba.
……………………………………………………………………………………
Wakazi
wa Kata mbalimbali za Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam wanatarajia
kunufaika na mradi wa maji safi na salama ya kunywa ifikapo mwezi
Disemba mwaka huu.
Mradi
huo wa maji ya visima unatekelezwa kwenye Kata tisa ambazo ni Magomeni,
Sinza, Manzese, Kinondoni na Kibamba, Msasani, Temboni, Mzimuni na
Msumi.
Akizungumza
wakati wa ziara yake ya kutembelea ujenzi wa miradi hiyo katika Kata
nne za Manzese, Sinza, Kinondoni Shamba na Magomeni, Meya wa Manispaa ya
Kinondoni Yusuf Mwenda amesema Manispaa yake imejipanga vema
kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ndani ya mwezi Disemba na kuwataka
Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kuisimamia ili ikamilike kwa
muda uliopangwa.
“Wito
wangu kwa Madiwani, Watendaji na Wenyeviti muhakikishe mnaisimamia kwa
nguvu zenu zote miradi hii ikamilike ndani ya muda tuliokubaliana na
wakandarasi ili wananchi waanze kunywa maji haya ndani ya mwezi
Disemba.” Alisema Meya huyo.
Aidha
amezionya Kamati za Maendeleo ya Kata na Kamati za Maendeleo ya Maji
kuhakikisha miradi hiyo inawanufaisha wananchi badala ya watu wachache
wenye tamaa na kuwataka Madiwani na Wenyeviti kulisimamia hilo.
Katika
ziara yake Meya huyo akiambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo
mbalimbali vya habari ilishuhudiwa baadhi yake ikiwa kwenye hatua nzuri
ikiwemo Mtaa wa Mivuleni, Kata ya Manzese ambapo ilishuhudiwa wananchi
wakianza kuchota maji ya Kisima kilichokuwa kwenye hatua ya mwisho ya
ujenzi wake.
Miradi
hiyo ya Maji safi na salama ya kunywa ya visima ni sehemu ya
utekelezaji wa ahadi ya Serikali ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwapatia
maisha bora watanzania chini ya Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Post a Comment