Mkono wa mtu uliopatikana kandokando ya Kiwanda cha kutengeneza mifuko ya Viroba na Plastiki, Mababi jijini Dar.
Dada wa kijana anayedaiwa kuwa mwenye mkono huo, Rehema Rashidi akihojiwa na mwandishi wa ITV, Sam Mahela.
Mmiliki wa kiwanda hicho, Lee Sliim, akiwa ndani ya gari la Polisi kuelekea kituoni kwa mahojiano zaidi.
DUNIA
inaimba sandakarawe! Mwenye kupata sasa anapata na mwenye kukosa hana
chake tena! Mwekezaji mmoja wa kiwanda cha Urafiki Plastic Co. Ltd
kinachokihusisha na utengenezaji wa mifuko ya viroba na palstiki ambaye
ni raia wa China, Lee Slim amekamatwa kwa tuhuma za kuonekana kwa mkono
wa mtu karibu na kiwanda chake, tukio hili limetokea mchana huu maeneo
ya Mabibo, jijini Dar es salaam. Mkono huiop unadaiwa kuwa ni wa
mfanyakazi wa kiwanda hicho, kijana Jumanne Rashid. ( HABARI/PICHA: BRIGHTON MASALU/GPL )




Post a Comment