MPANGO
wa Taifa wa Damu Salama Tanzania (NBTS) umevuka malengo ya ukusanyaji
damu kwa asilimia 110 katika kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi
Septemba 2013 ambapo jumla ya chupa 38,552 zilikusanywa na kuvuka
malengo ya chupa 35,000 zilizokuwa zikusanywe.
Ofisa
Uhusiano na Masoko wa Mpango wa Damu Salama Tanzania Bw. Rajab Mwenda
alisema Kanda iliyongoza kwa makusanyo ya damu ni Kanda ya Mashariki
inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam,Morogoro,Dodoma na Pwani ambako
jumla ya chupa 13,669 zilikusanywa, Kanda inayofuatia kwa ukusanyaji
damu ni Kanda ya Kaskazini (Kilimanjaro,Arusha, Manyara, Tanga)
iliyokusanya chupa 6,159.
Alisema
katika kipindi cha mwezi oktoba 2012 hadi Septemba 2013 takwimu
zinaonyesha chupa za damu 139,676 ambayo ni sawa na asilimia 99.8 ya
lengo la kukusanya chupa 140,000 ilifikiwa hata hivyo Mpango wa Taifa wa
damu salama unakusanya asilimia 26 ya mahitaji ya damu kwa mwaka.
Mahitaji ya damu kwa mwaka ni wastani wa chupa 400,000- 450,000.
Alisema
tofauti iliyoko ya upatikanaji wa damu kwenye hospitali nchini imekuwa
inafidiwa na ndugu wa wagonjwa katika kuchangia damu ili kuokoa maisha
ya mgonjwa.
Bw.
Mwenda alisema sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mpango kushindwa
kukusanya damu kwa 100% toka kwa wachangiaji damu wa hiari kunatokana na
uelewa mdogo katika jamii kuhusu uchangiaji damu kwa hiari kwani mfumo
uliozoeleka ni ndugu wa mgonjwa ndiyo wanatoa.
Alisema
nyingine ni uhamasishaji usiotosheleza toka kwa viongozi mbalimbali wa
jamii, wanasiasa, viongozi wa dini, uuzwaji wa damu usio halali
hospitalini jambo ambalo linawakatisha tamaa wachangia damu wa hiari,
matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na miundombinu hafifu
hususan barabara duni wakati wa kukusanya na kusambaza damu.
Bw.
Mwenda alisema Mpango wa Taifa wa Damu salama una wadau mbalimbali
ambao hujitokeza kuchangia damu kwa hiari kama taasisi za kidini,
majeshi, sehemu za kazi, mikusanyiko ya watu na wanafunzi ambao
huchangia asilimia 80 ya damu hapa nchini.
Alisema
katika kipindi cha Novemba hadi Januari kila mwakani ni kigumu katika
ukusanyaji damu kwani wadau wakuu ambao ni wanafunzi wanakuwa likizo ya
mwaka hivyo Mpango wa Taifa wa Damu Salama umeweka mikakati mbalimbali
ili kukabiliana na changamoto hiyo.
Alisema
katika mikakati hiyo ni kufanya kampeni ya kuhamasisha uchangiaji damu
kwa hiari katika jamii na sehemu za makanisani, minadani, stendi za
mabasi, misikitini, kwenye masoko na sehemu za kazi.
Alisema
wameanza kuhamasisha kambi za jeshi, makundi ya dini na ma wasiliano
yamefanyika kwa jumuiya mbalimbali hapa nchini zichangie damu mfano
jumuiya ya Khoja shia, Sabato na Jaula.
Pia
alisema watatumia vyombo vya habari ili kuikumbusha na kuielimisha
jamii juu ya umuhimu wa kuchangia damu na visaidie kutoa elimu na
kutangaza ratiba ya ukusanyaji damu katika vituo vidogo na vikuu.
Alitoa
rai kwa Watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa hiari katika vituo vya
damu salama kwa mtu yoyote mwenye afya mwanamke au mwanaume na mwenye
umri kuanzia miaka 18 ajitokeze kuchangie damu.
Alisema
uchangiaji wa damu kwa hiari una faida kwa mtoaji kwa vile napunguza
hatari ya magonjwa ya moyo, kuwepo kwa madini chuma mengi kupita kiasi
katika damu kunakodhoofisha utendaji kazi na kuchangia damu mara kwa
mara hurekebisha madini chuma ya ziada katika mfumo wa damu.
Alisema
faida nyingine ni upimaji wa afya pasipo gharama kwa sababu wakati
unapochangia damu mtaalamu wa tiba daktari au muuguzi atapima shinikizo
la damu yako, mapigo ya moyo na kukufanyia vipimo vya afya bure.
Alisema
kutoa damu kunaongeza utambuzi wa kiwango cha chembe hai nyekundu na
chembe na huchochea uzalishaji wa seli damu mpya na kuwaomba wanahabari
kuendelea kuhamasisha na kuielimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuchangia
damu kwa hiari mara kwa mara kwani ni damu ya mwanadamu pekee
inayotumika kumuongezea mgonjwa anayehitaji damu.
Post a Comment