Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSAFARA WA RAIS KIKWETE WAPATA AJALI MBAYA

Msafara wa Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Kikwete mkoani Geita, leo umeingia dosari baada ya gari moja lilokuwa kwenye msafara huo kupinduka na kujeruhi watu watano.

Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.


 

Askari akilikagua gari.

Mwandishi Peter Makunga akiwa anaendelea kupatiwa matibabu baada ya ajali hiyo, hospitali ya wilaya ya Geita.
Gari la Bohari ya Dawa (MSD) lililopata ajali likiwa na meneja wa MSD Kanda pamoja na waandishi wa habari.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Geita Lenard Paul ajali hiyo imetokea leo saa 3 na dakika 45 asubuhi katika eneo la Nyankumbu kilomita 3 kutoka makao makuu ya mkoa wa geita.

Kamanda Paulo amesema gari hilo namba DFP.9730 aina ya Toyota Landcruzer lililokuwa likiendeshwa Yungi Mkwati, mali ya Bohari kuu ya Madawa (MSD), lilipinduka baada ya kuteleza kwenye lami iliyomwagwa barabarani hii leo.

Amewataja Waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni mwandishi Peter Makunga wa Radio Kahama Fm na Radio Free Afrika, Peter Fabian wa Gazeti la Rai, Frederick Katulanda Moderator wa Tovuti ya mabadiliko.com, meneja wa MSD kanda ya Ziwa Byekwaso Tabura pamoja na dreva wa gari hilo Yungi Mkwati.

Kamanda Paulo amesema majeruhi wote wamefikishwa katika hospitali ya wilaya ya Geita kwa ajili ya matibabu na kisha kuruhusiwa huku Mwandishi Peter Makunga akiwa bado amelazwa hospitalini hapo na hali yake inaendelea vizuri.
source:faraji mfinanga.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top