**********
JESHI la Polisi mjini hapa, limemtia mbaroni mwanamke ambaye ni raia
wa Tanzania kwa kukusanya walemavu na kuwafanya kuwa kitega uchumi
chake. Kwa mujibu wa taarifa iliyotangazwa jana na Kituo cha Runinga cha
Citizen cha nchini Kenya, ilisema kuwa watu 26 walikamatwa akiwemo
mwanamke huyo kutoka Tanzania.
Mwanamke huyo amekuwa akienda kufanya biashara ya kuomba fedha na jioni amekuwa akipitia hesabu, huku akiwa amewaweka walemavu hao wakiishi kwenye nyumba moja katika eneo la Mwembetayari.
Mbali na hilo, anadaiwa kuwa na mtindo wa kuagiza walemavu kutoka Tanzania na kuwapitisha kupitia mpaka wa Taveta na Lungalunga, ambapo huwatumikisha kwa ajili ya biashara.

“Hadi sasa wamekamatwa washukiwa saba akiwemo yeye na mshirika wake kutokana na tukio hili,” kiliripoti kituo hicho cha runinga.
Taarifa inasema ombaomba hao wamekuwa wakichukuliwa kutoka katika mikoa ya Shinyanga, Mwanza na wilaya za Musoma na Bukoba, ambapo hupita katika mitaa ya Mombasa na kuomba na pindi wanapopata Sh 500 za Kenya tajiri huyo wa Kitanzania huchukua Sh 300 na kuwaachia Sh 200 kila mmoja.
Mmoja wa walemavu hao alisema kuwa: “Kabla ya kuletwa Kenya tunapewa ahadi nzuri za kuvutia kwenda, mimi niliahidiwa kupewa baiskeli lakini kinachotokea hivi sasa ni kwamba nikipata hiyo pesa ya kuombaomba, mwanamke huyu ndio anapanga bajeti zake wala hamna anachofanya,” alisema mmoja wa walemavu hao.
Hata hivyo RAI ilimpomtafuta Balozi mdogo wa Tanzania, Yahya Jecha, ili kuweza kuzungumzia jambo hilo muda wote simu yake ya mkononi iliita bila kupokelewa.
Pamoja na hali hiyo, juhudi za kuweza kumpata bado zinaendelea kufanyika ili kupata ufafanuzi wa sakata hilo.
RAI
Post a Comment