pix1
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza  Bwana Elias Musangeya (kushoto) alipotembelea Wizarani hapo kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration  leo jijini Dar es Salaam.
pix2
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya (kushoto) akielezea jambo  huku Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo (kulia) na Mshauri Mwandamizi wa UK Sports Elias Musangeya (katikati) wakimsikiliza kwa makini. Mkutano huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration.

pix3
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo (kulia) na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza  Bwana Elias Musangeya (kushoto) wakifurahia jambo walipokutana ofisini kwa Kaimu Katibu Mkuu huyo kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration  leo jijini Dar es Salaam.
pix4
Kutoka kulia Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo, Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza  Bwana Elias Musangeya, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo sehemu ya Usajili Bi. Mercy Rwezahura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha  tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Frank Shija – WHVUM).