| ***** |
Na Frank Mvungi-Maelezo
Mfuko
wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF) waanza kukopesha nyumba
wanachama wake ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha huduma zake kwa
wanachama.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa uendeshaji na
Meneja kumbukumbu wa mfuko wa Resheni kwa watumishi wa umma Bw. Chacha
Nyaikwabe wakati wa mkutano na waandishi wa habari .
Akifafanua
zaidi alisema mfuko huo umejenga nyumba katika mikoa ya Shinyanga
nyumba 50,Mtwara nyumba 50 na Morogoro nyumba 25 ambapo lengo la Mfuko
huo ni kufika mikoa yoye hapa nchini.
Aliongeza
kuwa nyumba hizo zinakopeshwa kwa wanachama wa mfuko huo ambao
wanatakiwa kulipa mkopo wa Nyumba hizo kwa muda wa miezi 300.
Alibainisha
kuwa hata wananchi wasio wanachama wanaweza kununua nyumba hizo ambazo
kila moja inagharimu kuanzia milioni 59 hadi milioni 80 kutegemeana na
ukubwa wa nyumba.
Alitoa
rai kwa wananchi wote kujiunga na mfuko huo bila kujali wako katika
sekta rasmi au isiyo rasmi ili waweze kunufaika na mafao mbalimbali
yanayotolewa na mfuko huo ikiwemo fao la elimu,Kifo, kujitoa na Ugonjwa.
Aliongeza
kuwa katika kuboresha huduma zake mfuko huo sasa umeanza kusajili
wanachama katika mpango wa hiari kwa raia na asiye raia wa Tanzania
ambapo mwanachama anaweza kuwasilisha michango yake kwa wiki, mwezi au
msimu.
Katika
hatua nyingine Mfuko huo umeanzisha utaratibu unaowawezesha hata wasio
wananchi walio nje ya Tanzania kujiunga na mfuko huo ilimradi tu wawe
watanzania.



Post a Comment