Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI
ya Clouds Media Group, imekuwa miongoni mwa wadau waliojitokeza
kudhamini Tamasha la Handeni, linalotarajiwa kufanyika Desemba 14 mwaka
huu na kusubiriwa kwa hamu wilayani Handeni mkoani Tanga nchini
Tanzania.
Kwa
sasa maandalizi kabambe yamekuwa yakipamba moto kwa ajili ya
kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika kwa mara ya kwanza katika
historia ya Taifa kwa mafanikio makubwa, sanjari na kutafuta mbinu za
kimaendeleo.
Akizungumza
jana jijini Dar es Salaam, Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo linalotambulika
pia kama ‘Handeni Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kuwa kuingia kwa
kampuni hiyo ni sehemu ya kulifanya tamasha hilo liwe na mvuto mkubwa
zaidi.
Alisema
kuwa juhudi zao ni kuhakikisha kuwa tamasha hilo linafanyika wilayani
humo na kushirikisha mkoa wa Tanga na Tanzania kwa ujumla, hivyo ni
wakati wa wadau wengine kujitokeza kuliwekea mguso wazo hilo.
“Tunashukuru
kuona Watanzania wote wanaingia humu ili wazo hili lifanikiwe kwa
kiwango kikubwa, ingawa tamasha hili linafanyika kwa mara ya kwanza
mwaka huu, huku likiwa na changamoto lukuki.
“Naamini
huu utakuwa mwanga mzuri kutoka kwa wenzetu Clouds Media Group ambao
pia wanamiliki redio ya Clouds FM na Clouds TV, huku wakiwa ni waandaaji
wa Tamasha kubwa la Fiesta linalofanyika kila mwaka na kuzunguuka mikoa
mbalimbali ya Tanzania na kukonga nyoyo za wapenzi wa muziki wa ndani
na ule wa Kimataifa,” alisema Mbwana.
Wadhamini
wengine ni Yusuphed Mhandeni, ambaye ni Mchumi wa CCM Kata ya
Makumbusho kwa kupitia Kampuni yake ya Phed Trans, Grace Products,
Screen Masters na mtandao wao wa Saluti5.com, Dullah Tiles &
Construction Ltd, Katomu Solar Specialist, Planbtz Country Business
Directory (CBD) na Michuzi Media Group.
Wengine
ni duka la mavazi la Chichi Local Ware, Smart Mind & Arters chini
ya Anesa Company Ltd, ikidhamini kwa kupitia kitabu chao cha ‘Ni Wakati
Wako wa Kung’aa’, Lukaza Blog, Kajunason Blog, Jiachie Blog na Taifa
Letu.com.
Post a Comment