Timu
ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza
raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada jana (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Mabao
ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto
jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu
(hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia
Minja.
Msafara
wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho Jumapili (Novemba 10
mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Tanzanite
inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili
dhidi ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam
kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika
Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Post a Comment